Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 26 YA 31

Petro, Yohana na Yakobo walipata upendeleo wa kuwa na Bwana wao alipokuwa anashindana na nguvu za kifo katika maombi. Aliwahimiza mara mbili waombe, lakini walilala. Katika jambo hili, Yesu alisisitiza umuhimu wa kukesha ili kutoingia majaribuni. Twahitaji kuongozwa na somo hili, kwani tumesongwa kila upande na mambo tusiyoyamudu sisi wenyewe. Jambo kubwa kuliko yote ni Ibilisi angurumaye akitafuta mtu ammeze. Hatuwezi kumshinda msaliti wetu, wala hatuna nguvu ya kustahimili majaribu bila kuwa waombaji.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz