Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 13 YA 31

Daudi alitaka Yerusalemu uwe mji mkuu kiroho pia. Lakini kabla ya kulipandisha sanduku la Bwana huko, Daudi alitafuta ushauri kwa Bwanana kwa wanadamu pia. Daudi akafanya shauri na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, na kila kiongozi.Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa Bwana, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hamkuuliza neno kwa hilo katika siku za Sauli.Nao jamii nzima wakasema ya kwamba watafanya hivyo; kwa kuwa neno hilo lilikuwa jema machoni pa watu wote(1 Nya 13:1-4). Utaratibu huo pia ni muhimu kuufuata kwa kiongozi wa kanisa akitaka kutenda jambo la pekee. Pasipo mashauri makusudi hubatilika; bali kwa wingi wa washauri huthibithika(Mit 15:22). Mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika(Mit 16:3). Ila katika jambo lingine Daudi alikosa. Hakufuata maagizo ya pekee katika sheria ya Bwana yahusuyo uhamisho wa sanduku la Bwana (Hes 4:15, Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife). Kwa hiyo ikatokea ajali, na Uza akafa papo hapo kwa pigo la Bwana!

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz