Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 12 YA 31

Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi (m.17). Huko mwanzo Daudi alijulikana kwa Waisraeli kwa sababu ya kumshinda yule Mfilisti Goliathi. Alikuwa amemtegemea Bwana peke yake, na Bwana alimpa ushindi wa ajabu. Leo tunaona kuwa Daudi bado ana moyo huo huo. Mara mbili twasoma Daudi akauliza kwa Bwana (m.19, 23). Na alipokuwa ameshinda, alijua ni ushindi wa Bwana wala si ushindi wake: Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu (m.20; ling. m.24). Fundisho: Tuwe na utii na unyenyekevu mbele ya Bwana! Je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu(1 Sam 15:22).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz