Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano
Daudi aliipiga ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi (m.7). Sayuni ni sawa na Yerusalemu. Daudi aliufanya mji huo kuwa mji mkuu wa ufalme wake badala ya Hebroni. Ni kwa sababu Daudi sasa hakuwa mfalme wa kabila la Yuda tu bali wa makabila yote(m.1-3). Alitaka kuwakusanya Waisraeli wote bila upendeleo. Mji huu ulikuwa katikati ya nchi. Eneo la Yerusalemu lilikuwa limebaki kutawaliwa na wapagani tangu wakati wa Yoshua. Hao wakimwambia Daudi katika m.6-8 kwamba vipofu na viwete wangeweza kuilinda ngome ya Sayuni, ni sawa na kusema uimara wa ngome ni kubwa kiasi cha Daudi kushindwa kuiteka. Katika 1 Nyakati 11:4-9 kuna habari zaidi jinsi Daudi alivyoweza kuiteka. Ila sababu hasa inaelezwa katika m.12: Akajua Daudi ya kwamba BWANA amemweka imara awe mfalme juu ya Israeli, na ufalme wake ameutukuza kwa ajili ya watu wake, Israeli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz