Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano
Daudi anaonyesha jinsi Mungu wa kweli alivyo mkuu, na jinsi Mungu anavyowapenda watu wake na kujibu maombi yao. Tena mataifa yote yangepaswa kumjua mwenyezi Mungu, kwa sababu hakuna Mungu mwingine (m.4-5: Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako. Naam, wataziimba njia za Bwana, Kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu). Neno la Mungu linaleta matumaini na ahadi ya kuokolewa kwa watu wote duniani. Anajua kwamba Mungu daima atakuwa mwaminifu kwa kutimiza ahadi yake ya kumwokoa. Utukufu wa Mungu na neno lake linamletea Daudi matumaini, hata wakati wa mateso na shida. Kwa kweli: fadhili za Mungu ni za milele!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz