Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/20

SIKU 20 YA 29

Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? (m.11) Swali hili liliulizwa na Mafarisayo walipoona Yesu ameketi nyumbani kwa Mathayo pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi. Baadaye huyu Mathayo akawa mtume, na ndiye aliyeiandika Injili hii tusomayo. Yesu alijibu swali, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi(m.12-13)! Yesu hakula nao ili kushirikiana nao katika maovu yao, bali kwa sababu aliwapenda. Ni wenye thamani kubwa kwa Mungu. Kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu(Lk 15:7). Alitaka awaokoe. Je, sisi Wakristo tunawapenda wasiomjua Mungu?

Andiko

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz