Soma Biblia Kila Siku 10Mfano
Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja (m.14). Hapa Paulo anawafananisha Adamu, mtu wa kwanza duniani, na Yesu Kristo, Adamu wa mwisho (1 Kor 15:45: Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho [Kristo Yesu]ni roho yenye kuhuisha). Wanafanana kwa njia mbili: Moja, wote wawili ni wanadamu (m.15: ...kipawa kilicho katika neema yake mwanadamummoja Yesu Kristo kimezidi...). Pili, waliyoyafanya walifanya kwa niaba ya wanadamu wotewa vizazi vyote (m.18-19:Kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki)! Yaani Adamu kufanya dhambi kuliwafanya wanadamu wote wawe wenye dhambi na mwisho kufa. Na Kristo kuondoa dhambi kumewawezesha wanadamu wote kupata msamaha wa dhambi na mwisho uzima wa milele kwa kupokea zawadi hii kwa imani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz