Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 31 YA 31

Leo twapata faraja nyingine ya nne zaidi ya hizo tulizozikumbushwa jana: Katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema (m.28).Kama ni maudhi au ni ugonjwa au ni ajali au taabu ya aina yoyote, haya yote tuyapokee mikononi mwa Mungu kwa imani tukijua kwamba anao uwezo wa kutupatia mema hata kwa njia ya mambo yasiyomema! Mistari ya 35-37 inaonyesha ni kwa jinsi gani: Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.Mkazo wa Paulo ni katika neno hili twajua(m.28). Hata tusipoelewa au kujisikia kuwa tukio fulani litatupatia mema, tusiwe na mashaka maana twajua! Usiogope, amini tu(Mk 5:36). Shabaha kuu ya Mungu ni kwamba tutukuzwe! Wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza (m.29-30).

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz