Soma Biblia Kila Siku 10Mfano
Katika m.17-18 Paulo anakumbusha kuwa ni kawaida Wakristo kuteswa pamoja na Yesu kwa sababu ya imani yao na msimamo wao katika yeye (ling. 2 Tim 3:12 anaposema kuwawote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa). Lakini tusikate tamaa, bali tuvumilie, maana: 1.Utukufu ule utakaofunuliwa kwetuatakaporudi Yesu ni mkubwa na wa ajabu (m.18). Hiyo tunajua na kutajaria kwa sababu tayari tumepewa malimbuko yake ambayo ni Roho anayekaa ndani yetu (m.23). 2. Uumbaji wote wa Mungu unaugua pamoja na sisi! Nao pia utaondolewa laana na kuwekwa huru atakapokuja Yesu (ukitaka kujifunza zaidi juu ya jambo hili, soma Isa 11:6-9, Kol 1:19-20 na Ufu 21:5). 3. Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu hutuombea kwa nguvu kwa Baba.Kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba(Gal 4:6). Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz