Soma Biblia Kila Siku 10Mfano
Kufanikiwa kuna hatari, nayo ni kiburi! Tazama m.6 ambapo Mwimba Zaburi anasema kama mpumbavu:Nilipofanikiwa nalisema, Sitaondoshwa milele(ling. Zab 10:6 ambapo mtu anasema vivyo hivyo:Sitaondoshwa, kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni). Kwa hiyo akapatwa na hasira ya Mungu, akataka kufa. Lakini akagundua kuwa hasira ya Mungu kwa watu wake ni ya kitambo, yaani, inadumu mpaka tuombe radhi kwake:Ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, katika radhi yake mna uhai(m.5). Je, unajua kuwa tunaishi kwa sababu Mungu anatulinda na kutuepusha na kifo? Au kwamba kama tukifanikiwa na kuinuliwa katika maisha, ni kwa sababu ya wema wa Mungu? Tumshukuru Mungu kwa mema mengi tupatayo maishani ili tusijivune na kufa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz