Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 29 YA 31

Katika Imani ya Mitume twakiri "ufufuo wa mwili". Tumaini hili la uzima wa milele twaona katika m.17: Tu warithi ... warithio pamoja na Kristo. Kumbuka pia m.10-11: Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Pia tunazidi kufundishwa juu ya maisha yenye ushindi katika m.13 ilipoandikwa kuwa mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi."Mwili" ni utu wa kale, ni ule uadui juu ya Mungu ambao hauwezikumtii Mungu (m.7). Matendo yake ni matendo ya dhambi na yanafishwa kwa Roho pale tunapomtazama Yesu kwa imani ambaye amekwisha yachukua msalabani! Sidaiwi na dhambi (m.12) bali ni mtoto wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba(m.15)!

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz