Soma Biblia Kila Siku 10Mfano
Ole wangu, maskini mimi! ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu (m.24-25). Mapambano haya katika maisha ya Mtume Paulo yanaonyesha kuwa Roho Mtakatifu yuko maishani mwake, maana kwake Paulo dhambi imekuwa ni kitu kibaya! Anaichukia. Katika 1 Yohana 1:7-9 tunapewa ufafanuzi mzuri wa hali hiyo: Tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Mapambano ndani ya Mkristo ni kati ya utu wa kale (mwili wa mauti) na utu mpya (Roho Mtakatifu). Namna ya kushinda katika mapambano haya Paulo anatufundisha katika sura za 6 na 8. Tutashinda kwa Yesu Kristo Bwana wetu(m.25)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz