Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Katika somo la leo tunapata mialiko miwili: Katika m.1-6 ni Hekimaanayetukaribisha kwenye karamu ya Ufalme wa Mungu ili tukafurahie mema yote ya uzima atukirimiao. Katika m.13-18 ni Upumbavuanatukaribisha kwenye karamu yake yenye wizi na siri. Wageni wake wanaingia mautini. Heri anayeitikia wito wa m.6! Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, mkaende katika njia ya ufahamu. Lakini tufanyeje na mtu yule asiyetaka? Angalia m.8-9: Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu. Yesu alisema vivyo hivyo katika Mt 7:6, Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Tunafanya vema tukiwaombea wasiotaka, lakini tusiwasumbue kwa maonyo endelevu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
