Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 7 YA 31

Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo (m.7). Bwana alimtafuta mtu ambaye anampenda kwa moyo ili awe mfalme badala ya Sauli. Akamchagua Daudi, mwana wa Yese, aliyekaa katika kijiji cha Bethlehemu. Kati ya wana wanane wa Yese, Mungu akamchagua mdogo kuliko wote. Tunapowachagua viongozi katika kanisa, tuzingatie fundisho alilopewa Samweli siku ile! Tumwombe sana Bwana atuongoze tuchaguapo. Yeye ndiye ajuaye mioyo ya watu! Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile(m. 11-13).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz