Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 22 YA 31

Mtu ambaye amefungwa na torati au sheria ya Mungu yukoje? Ni mtu ambaye ameutambua utakatifu wa Mungu na kuamini kwamba kwa kujitahidi kutenda mema ataweza kupata kibali cha kuingia Mbinguni. Ni mtu anayehangaika sana, maana anapokazana kushinda dhambi, hiyo dhambi inazidi tu kumtawala, maana inatoka ndani ya moyo wake (m.5: Tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao.Yesu anatukumbusha viyvo hivyo katika Mk 7:21-23: Ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi). Kwa hiyo mtu aliyefungwa na sheria ya Mungu, akitegemea itamsaidia kuwa mtakatifu machoni pa Mungu, anazidi kuogopa hasira ya Mungu. Lakini akitambua kwamba Kristo badala yake amekwisha timiza madai yote ya Mungu, mara hufunguliwa na kuzaliwa kwa Roho (m.4:Ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda. Na m.6: Tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho).

Andiko

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz