Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Ndugu Mkristo, usikubali kutawaliwa na dhambi! Tuliona jana kuwa dhambi haina haki tena kukutawala. Maana umekufa pamoja na Kristo na umefufuka pamoja naye. Umepata maisha mapya (2 Kor 5:17: Kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu. Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu). Unajua kwamba utu wako wa kale (utu wa dhambi) ulisulubishwa pamoja naye, ili usitumikie dhambi tena (m.6: Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena). Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai (m.12-13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
