Soma Biblia Kila Siku 10Mfano
Malaika wanapewa wito na Mwimba Zaburi kumwabudu Bwana, na kulisifu jina lake kwa kuwa uwezo wake ni mkuu. Uwezo wake huo umedhihirishwa na sauti yake itendayo maajabu. Ina nguvu ya kupiga kama radi na hata kuivunjavunja mierezi ya Lebanoni. Huleta uhai na kusababisha waabuduo katika hekalu la Mungu kuona utukufu wa Bwana (m.3-9). Naam, na uumbaji wote hutegemea Neno lake, maana Mungu alisema viwepo, vikawa. Zaburi inatukumbusha jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu, k.m. Mwa 1:3 ilipoandikwa: Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu yu mfalme milele, na anastahili kuabudiwa. Heri wale ambao nguvu yao ni Bwana!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz