Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha YakoMfano
Ukiwa nyumbani au kazini, ukiwa sehemu ya kundi la marafiki au familia, wote tumejifunza jinsi ya kutunza na kurekebisha tabia zetu.Kaa sawasawa. Sema tafadhali. Vaa hiki. Fanya hivyo.
Bado, mara moja baada ya muda, tunasema au kufanya mambo yasiyoleta maana. Ni kama vile kutapika--labda ni kusema kwa hasira au hamaki za uchungu. Tunaweza hata kusema baadaye, " Sijui yalitoka wapi!"
Lakini tunajua, kama tuko wawazi na jasiri kukabiliana nayo. Inatoka ndani yetu. Yesu na Mfalme Sulemani wanatuambia kile kilicho mioyoni mwetu ndicho tatizo.
Tunahitaji vizuia njia kwa ajili ya mioyo yetu. Kwa sababu, mwishowe, tabia zetu (Kwa nje) zitaonesha kile kinachoendelea ndani.
Kuna hisia nne ambazo zinatakiwa akupiga kengele katika fahamu zetu. zinatakiwa zitufanye kusimama na kujitazama ndani kuangalia nini kinaendelea ndani ya mioyo yetu. Ni hukumu, hasira, uchoyo na wivu.
Hukumu inasema, "unanidai." unanidai kitu kwa sababu nilichukua kitu kutoka kwako. Kuondoa hukumu, unatubu. Tubu kwa mtu; ili ajue.
Hasira inasema, "Nakudai." Uliniumiza au ulichukua kitu changu. Kuondoa hasira, ni kusamehe. Kumsamehe mtu unayemdai. Waondoe katika ndoano.
Uchoyo inasema, "Ninajidai." Uchoyo ni kudhani vyote ni kwa ajili ya matumizi yangu. Kuondoa uchoyo, ni kutoa. Kuwa mkarimu. Bila kutegemea chochote. Bila kutaka sifa.
Wivu inasema, "Maisha nayadai." Mtu mwingine anacho/ nachostahili. Kuondoa wivu, furahia cha mtu mwingine. Waandikie ujumbe. Wapongeze juu ya kitu kile ambacho unakionea wivu.
Tunapokutana na vizuia njia hivi vya hisia, tunahitaji kuwa makini sana. Vinaashiria hatari. Ukidharau maonyo hayo utajikuta upande wa pili.
Kama umefurahia mpango huu, angalia jumbe tano za video za Andy Stanley's kuhusu vizuia njia-- na video nyingine nyigi za masomo ya Biblia kwenye http://anthology.study.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi.
More