Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha YakoMfano

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

SIKU 3 YA 5

Sisi wote tunamjua mtu, ni watu, au tutamwinua mtu ambaye maisha yake yatakuwa tofauti kabisa kama watakuwa wameweza vizuia njia kuongoza maadili ya ngono.

Kufanya hivyo siyo uchaguzi maarufu. Kusema ukweli, hakuna popote pale ambapo utamaduni unafanya kazi nzuri ya kutuongoza kwenye kingo ( na kuturudi na kutuaibisha tunapokosea) kuliko inapokuja kwenye mipaka ya maadili. Tunaangalia sinema, kusikiliza nyimbo, na kusoma vitabu vinavyotukuza ngono nje ya ndoa. Tunajiburudisha navyo wakati wote. Lakini inapotokea kweli... wakati mtu tunayemjua ana mahusiano? Wote tunashangaa.

Kwa hiyo, tahadhali nzuri: utamaduni utakuwa unapingana na juhudi zako za kuweka vizuia njia. Lakini katika mstari wa leo, mtume Paulo anaeleza kwa nini ni vya muhimu.

Anasema kukosa maadili ya kingono yanauharibifu sana. Kwa kweli, anaweka katika kundi lake tofauti, kusema hiyo ni kutenda dhambi " kwa mwili [wako]". Kwa maneno mengine, ni mbaya kwa mtu mwingine anayehusikana ni mbaya kwako. Na, kilcho zaidi, huwezi kukwepa matokeo yake. Unaweza kurejea kikamilifu kifedha. Unaweza kurejea kikamilifu kimasomo. Lakini inapokuja kwenye dhambi ya uzinzi, hakuna kurejea.

Kwa hiyo, ushauri wa Paulo ni nini? "kimbia . . ." 

Sicho kila mume anataka mke wake afanye? Kila mke anataka mume wake afanye? Kile kila kaka angetaka dada yake afanye? "Ikimbie zinaa. "

Tunamwekeaje mtu huyo vizuia njia? Hebu tuangalie jinsi Yesu alivyoelezea dhambi, Na ndipo tutaona jinsi inavyotumika kwenye dhambi ya zinaa. Katika huduma yake yote, Yesu alifundisha kile kilicho bora kwa watu wengine ndicho kilicho bora. Dhambi, ndiyo, kitu chochote kilicho pungua katika hilo. Kila mara nikiji wekambele yako kwa hasara yako, hiyo ni dhambi.

Kwa hiyo, vizuai njia kwa ajili ya ngono vituzuie kufanya chochote ambacho si bora kwa mtu mwingine. Watajisikia aibu? Itakuwa siri watakayobeba maisha yao yote? Itashusha mahusiano yao yote mbeleni? Ndipo, kama Paulo alivyosema, "kimbia."

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Andy Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.anthology.study/anthology-app