Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha YakoMfano

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

SIKU 2 YA 5

Majuto yetu makubwa mara nyingi yanahusiana watu tuliowahesabu marafiki. Yawezekana ya kwako yanahusiana na wenzako, mliosoma nao, au rafiki yako wa zamani wa kiume. Yawezekana ni kundi la marafiki ambao, unaomba, usingekutana nao. Hata kama ulikuwa peke yako, nafasi ni majuto yako makubwa ni kutokuwa na mahusiano.

Hawa marafiki wa uongo wametufundisha ( mara nyingi kwa njia ngumu) kwamba maisha yetu ya mbele yanaathiriwa na watu tunaokaa nao muda mwingi. Ndiyo maana tunahitaji vizuia njia vya hekima. 

Sulemani, mmoja kati ya wenye hekima ambao wamewahi kuwepo, aliandika " Tembea na wenye hekima upate hekima ..." Kwa maneno mengine, hekima huambukiza. Fanya maisha na wenye hekima na, baadaye, utakuwa na hekima. Inatokea moja kwa moja.

Na kuna sehemu ya pili: " ...k wa maana ushirika wa wapumbavu huumiza." Unapokaa na mpumbavu, unajikuta katika matokeo maamuzi mabaya. Unapata kibamba. Heshima yako inaharibiwa kama yake. Unafukuzwa kwama yeye. Wala hualikwi tena.

Vizuia njia vya busara vinatusaidia kuepuka " kushindwa kwa kijinga."

Kwa hiyo, unapofikiria kuhusu urafiki, hapa kuna vizuia njia vya kufikiria. Wakati moja ya mambo haya yanatokea, hebu viamshe dhamira kabla ya kuumia.

1. Unajikuta unajifanya kuwa mtu fulani kuliko uhalisia wako

2. Kitu ambacho hakijawahi kuwa jaribu na sasa unakifikiria.

3. Unatarajia watu unaowajali hawajui ulipo.

Kumbuka, vizuia njia haviwekwi kutangaza kitu ( au mtu) sahihi au makosa. Vinakusudiwa kukurudisha katika hekima. Kwa hiyo, kuna rafiki yako akielekea sehemu hatari? Vizuia njia gani unavigonga na utafanya nini kuhusu hilo?

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Andy Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.anthology.study/anthology-app