Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha YakoMfano

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

SIKU 4 YA 5

Unapofikiria vizuia njia vya kiuchumi, unaweza kufikiria kuwa bila madeni. Kuwa bila madeni ni jambo jema, lakini kulingana na Yesu, unaweza usiwe na madeni na una fedha nyingi benki na bado ukawa katika shimo kifedha. Inachanganya, siyo? Endelea kusoma.

Katika mstari wa leo kutoka Mathayo, Yesu anasema sisi wote tunatawaliwa (au kumilikiwa) na mtu au kitu. Ndipo anatupa machaguo mawili: Mungu au fedha. Wengi wetu tungetarajia atuambie kwamba tutatawaliwa na Mungu au shetani. Lakini Yesu anasema mshindani wake mkuu ni fedha zetu.

Kimsingi anatutupia swali: Tunamiliki fedha au fedha zinatumiliki? 

Pasipokuwa na vizuia njia vya kifedha, wengi wetu tiutaishia katika moja ya mashimo hayo. Tutaserereka kwenye kilima cha matumizi au tutaanguka katika mpango wa kuweka akiba. Mojawapo ni shauku ya matumizi yasiyozuiliwa: nunua, boresha, rudia. Nyingine ni hofu isiyozuilika: Itakuwa kama sina fedha ya kutosha? Je hili likitokea kwangu?

Katika hali zote, fedha ni bwana wetu. tunazifukuzia ili tuweze kuzitumia sasa. au tunazifukuzia ili tuweze kuweka akiba na kuzitumia baadaye.

Tunahitaji vizuia njia vya kifedha vinavyomfanya Mungu Bwana wetu. Na hicho ndicho tunachokiopna katika Mathayo 6:33, kikishonwa mwisho wa mazungumzo marefu ya jinsi tunavyotakiwa kuona na kutumia fedha zetu. Ni maneno matano tu: "utafuteni kwanza ufalme wa Mungu."

Ufalme wa Mungu ni ufalme wa kwanza kwa wengine. Au kutumia maneno hayo hayo kama jana: katika ufalme wa Mungu, kilicho bora kwa wengine ndicho kilicho bora. Vizuia njia vitakavyotukinga na shimo la matumizi na kuweka akiba ni kuwaweza wengine kwanza katika fedha zetu.

Wape wengine kwanza. Weka akiba kwa baadaye kifuate. Ndipo, uishi kwa kilichobaki.

Toa kwanza. Tunza. Ishi kwa kilichobaki.

Na hapa kuna habari njema kuhusu vizuia njia: vinaweza kuwa automatiki. Utakapokuwa umesha chagua taasisi au kusudi unalolipenda na kuweka mfumo wa kutoa, kizuia njia hiki kitatunza fedha zako katika njia sahihi pasipokuwa na kazi kubwa au mawazo.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Andy Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.anthology.study/anthology-app