Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Vuzuia njia: Vinazuia Majuti Katika Maisha YakoMfano

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

SIKU 1 YA 5

Hakuna anayependa kuharibu maisha yao zaidi kuliko wanavyoharibu magari yao. Barabarani, tuna vizuia njia kutuzuia kuingia sehemu za hatari au nje ya barabara. Je, ingekuwaje kama tungekuwa na vizuai njia vinavyoweza kufanya kazi hiyo katika maisha yetu?

Baadhi ya majuto yetu makubwa yangeweza kuzuiliwa au kupunguzwa kama tungekuwa navyo Kwa ajili ya fedha zetu, mahusiano yetu, maadili yetu, na mihemko yetu.

Vizuia njia binafsi ni viwango vya tabia ambavyo vinakuwa mambo ya dhamira. Ni sheria unazojiwekea ambazo zinaamsha dhamira yako unapokutana navyo. Kama vizuia njia katika barabara kuu, vinawekwa sehemu ambazo bado ni salama. Muda mrefu kabla hujaharibu kazi yako, vizuizi binafsi vinatakiwa kukwambia unaelekea kwenye matatizo. Hata kabla hujasema huwezi kugeuza, vizuizi binafsi vinatakiwa vikuonye kuchunguza maneno yako kwa uangalifu.

Mtume Paulo anatupa ushauri mzuri tunapoanza kuweza vizuia njia vyetu: " Iweni waangalifu jinsi mnavyoenenda- si kama wasio na hekima bali wenye hekima..."

Mtume Paulo alijua ( na yawezekana umapata uzoefu) kwamba unaweza kuishia kubaya pasipo kuvunja sheria zozote. Unaweza kupoteza fedha pasipo kutumia isivyo halali. Unaweza kuharibu mahusiano pasipo kufanya chochote kilicho dhamba.

Vizuia njia haviwekwi tuu kukulinda upande salama wa makosa dhidi ya usahihi. Vinawekwa kukuweka katika upande wa hekima

Kwa hiyo, hapa kuna swali tutakalolitumia kwenye fedha zetu, mahusiano yetu, maadili yetu, na hisia zetu katika siku chache zijazo: Kutokana na uzoefu wangu, mazingira yangu ya sasa, na matumaini yangu na ndozo zangu za baadaye, ni jambo gani la hekima kufanya?

Katika ndoa yako...k atika kazi yako...i takapokuja kwenye suala la uishi wapi au utumieje muda wako... Ni jambo gani la hekima kufanya?

Swali hilo lingebadirishaje uchaguzi au hali ya zamani unayoijutia? Ingekusaidia wapi leo? Kama unaishi karibu na mwisho wa kingo, inaweza kuwa ni wakati wa kuweza vizuia njia.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Guardrails: Avoiding Regrets In Your Life

Vizuia njia vinawekwa kwa ajili ya kuyafanya magari yetu yasiende kwenye eneo la hatari. Mara nyingi hatuvioni mpaka tunapovihitaji-na hakika tunashukuru kuwepo kwake. Je ingekuwaje kama tungekuwa na vizuia njia kwenye mahusiano yetu, fedha zetu, na taaluma zetu? Vingeonekanaje? Vingetuzuiaje kutokana na kujilaumu baadaye? Kwa siku tano zijazo, hebu tuangalie namna ya kuweka vizuia njia binafsi.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya North Point Ministries na Andy Stanley kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.anthology.study/anthology-app