Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisiMfano

Not Forsaken: Finding Freedom as Sons & Daughters of a Perfect Father

SIKU 5 YA 5

Siku 5:

Fikiria juu ya wakati ambao unachoma nyama wakati wa kiangazi. Je, unaweza kunusa harufu ya nyama hiyo unayochoma? Labda usiku ufikapo utaongeza karoti ya marshmallow kwenye moto

Sasa fikiria kwamba una shida moja ndogo tu...huna meno! Hutaweza kuonja na kula hiyo nyama tamu uliyochoma mpaka umekomaa kua na meno ili uweze kuonja na kukula nyama hiyo na karoti ya marshmallow uliyochoma

Maisha yetu ya kiroho yanaweza kua hivi! Tunaweza kwama au kosa fursa maishani mwetu kama hatujakomaa

Unaona, Mungu hutumwagia baraka kama Baba yetu na pia hutusihi kufuata maisha yake. Anatusihi tuendelee kukomaa kwa kufuata maisha yake. Pamoja na kitambulisho chetu na nasaba yetu ya kiroho, tunaitwa kukua kama Baba yetu aliye mbinguni. Waefeso 5:1 inasema "Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa"

Tunaalikwa na tunaitwa kua kama Baba yetu. Tunamwangalia na tunaona jinsi Anavyofanya mambo yake - Anavyoongea, Anavyotembea na Anavyojibu. Tunaweka miguu yetu na kufuata nyayo Zake

Kinachostaajabisha ni kwamba Mungu hajatuacha peke yetu tufikirie tutakavyofanya; Anatupa kipawa cha Roho Mtakatifu wake kutuongoza na kutuelekeza. Kama Baba yetu asiye na kosa, Mungu hujihusisha katika maisha yetu. Anatuambia mimi na wewe, "acha nikuonyeshe utakavyofanya jambo hilo"

Kuna mambo matatu ya kufikiria, na kujielekeza, tunapomuiga na kukua katika maisha yetu ya kiroho.

1. Amka:kwa sisi ni nani na ni wa nani. Kama wimbo maarufu wa ibada unavyosema, sisi si watumwa tena..wa kuachwa, kuogopa, kutostahili, ukosefu wa usalama, kudhulumiwa, kulevya, hofu, kulinganisha au upweke...sisi ni watoto wa Mungu!

2. Kubali: matokeo ya vinasaba vipya. Tunaacha dhambi zetu na mwelekeo wetu wa zamani na kukimbilia mambo mapya na mazuri ambayo Mungu anatuita tufanye.

3. Kuasiri: tabia na nafsi za Mungu. Soma kwa undani jinsi Mungu anavyotembea na kufanya kazi zake. Pokea neno lake. Iga tabia zake na mwelekeo wake.

Umepitishwa na kuchukuliwa kama mtoto wa Mungu anayetupenda na asiye na kosa - sasa nenda uwe kama Baba!

Kuhusu Mpango huu

Not Forsaken: Finding Freedom as Sons & Daughters of a Perfect Father

Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha - kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake.

More

Tunapenda kuwashukuru Lifeway Christian Resources kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://notforsakenbook.com/