Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisiMfano
Siku 1:
“Baba, niangalie!”
Yawezekana ulisema maneno haya- au yanayofanana na hayo-ulipokuwa mtoto. Ni lugha ya kawaida kwa watoto, kelezea shauku yetu ya kutaka kuangaliwa, kuruhusiwa na kukubaliwa na baba zetu. Ikiwa ni kugongelea msumari kwenye ubao, kucheza michezo ya bunduki, au kucheza karata, tulitamani kusikia akisema "Ninakupenda na najivunia"
Dk. Peggy Drexler aliandika kuhusu shauku hii katika kitabu cha Saikolojia Leo utafiti wa wanawake 75 wenye mafanikio. Haijalishi wamefanikiwa kiasi gani kwenye taaluma zao, au maisha yao yamewatosheleza kiasi gani, wanawake waliniambia furaha yao ilipita katika chujio la baba zao.....hata kwa wanawake ambao baba zao walikuwa hawawajali au wadhalilishaji, nilipata njaa ya kukubaliwa.”
Katika kitabu chake, Mwanaume Kamili, Dk. Frank Pittman anaelezea njaa hiyohiyo ya kukubaliwa kwa wanaume: “Maisha kwa watoto wengi wa kiume na wanaume wengi ni kumtafuta baba ambaye hajatoa ulinzi, mahitaji, malezi, mfano, au hasa hasa upako.”
Neno "upako" linamaanisha kuchaguliwa, kubarikiwa....kukubaliwa. Inaonesha kitu cha thamani katika maisha yetu kinachofanya wote tutfute kukubaliwa na kutamaniwa na baba.
Yawezekana baraka hiyo imekuwepo katika maisha yako. Kama ni hivyo, chukua muda leo kama unaweza umwambie baba yako jinsi unavyomshukuru kwa ajili yako! Kama hauko hivyo, hauko peke yako. Kulingana na Taasisi ya Utafiti ya Marekani, zaidi ya mtoto mmoja kati ya wanne ya watoto wa Marekani leo wanaishi bila baba zao majumbani. Mara nyingi, "kutamani", " kukubaliwa," au " kuafiki" yatakuwa maneno ya mwisho kumwelezea baba. Maneno ambayo kwa haraka yatatujia akilini mwetu ni:
Hayupo.
Amekasirika.
Dhalilisha.
Mbali.
Ndiyo maana kizazi hiki kimepewa jina la "wasio na baba."
Lakini kuna jema, habari njema kwetu sote leo. Haijalishi tabia ya baba yako wa duniani ikoje, au hali ya uhusiano wako na yeye, kuna Baba halisi anayetaka kuwa na uhusiano na wewe. Tayari una mahaba yake. Tayari una mapenzi yake. Anakusubiri akumwagie baraka. Yeye ni kila kitu ulichokitaka kwa baba yako wa duniani kuwa na zaidi.
Katika siku tano zijazo, tutaona jinsi tunavyoweza kupata uhuru kama watoto wake wapendwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha - kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake.
More