Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisiMfano

Not Forsaken: Finding Freedom as Sons & Daughters of a Perfect Father

SIKU 2 YA 5

Siku 2:

Unawaza nini unapofikiria juu ya Mungu?

Mwanatheolojia A. W. Tozer alisema kwamba jibu la swali hili ni kitu cha muhimu sana kwetu. Kwa hiyo, Unawaza nini unapofikiria juu ya Mungu?

Wengine wetu tunadhani Mungu yuko, lakini hajihusishi sana na maisha yetu. Aliumba dunia na kumaliza, ndipo akakaa na kuangalia jinsi inavyojiendesha.

Wengine wanafikiria kwamba Mungu ni mtu fulani mzuri anayetaka na sisi yuwe wazuri na kuwa na maisha mazuri, lakini ni mgumu kusikiliza, hashikiki na kimsingi ni dhaufu sana kufanya kitu kikubwa.

Na watu wengine wanafikiria Mungu ni mkatili, anayependa kuuwa na yupo tuu kutuambia kile ambacho hatuwezi kukifanya.

Haya, na taswira zingine za Mungu ni vitu vya kawaida, lakini siyo sahihi. Unaona, Mungu si msimamizi wa miali ya jua mawinguni, Babu yako asiyekusikiliza, au nguvu ya uasi. Yeye ni Baba yetu. Maandiko yote, Mungu anahusishwa nasi kama Baba. Yesu mwenyewe, katika injili nne - Mathayo, Marko, Luka na Yohana-zinamtaja Mungu kama Baba mara 189. Ni wazi, ni muhimu tumuone na kuhusiana na Mungu kwa njia hii.

Lakini hiyo unaleta swali la pili. Unawaza nini unapofikiria juu ya Baba?

Uzoefu wetu, mzuri au mbaya, na baba zetu wa duniani sana sana unategemea tunajibuje swali hili. Kwa sababu hiyo, "Baba" yaweza isionekane ni jina zuri sana kwako zaidi ya "mtu anayeharibu furaha ya wengine" "asiyesikiliza" au "nguvu kutoka mawinguni." Lakini, pamoja na uzoefu wetu wa baba zetu wa duniani, wote tumeona shauku ya baba halisi.

Fikiria kuhusu shauku hii. Siku zote ulitamani baba yako awe ni wa namna gani?

Hapana kuna kitu cha kushangaza na habari njema kwako: Mungu ni Baba halisi. Yeye si baba mkubwa wa baba yako wa duniani, ni Baba halisi. Yeye ni jibu kwa kila shauku ya kukubaliwa na baba, kusaidiwa na upendo ambao umeuona.

Hii ina maana kwamba kila mmoja wetu--haijalishi uzuri, kutokuwepo, udhalilishaji, au kiukosekana baba zetu wa duniani walivyokuwa au walivyo-- tuna nafasi ya kuishi kama watoto wapendwa wa Baba halisi. Tukimuona Mungu kwa jinsi hii kuna nguvu ya kubadilisha uhusiano wetu na yeye, na baba zetu wa duniani.

Kuhusu Mpango huu

Not Forsaken: Finding Freedom as Sons & Daughters of a Perfect Father

Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha - kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake.

More

Tunapenda kuwashukuru Lifeway Christian Resources kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://notforsakenbook.com/