Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisiMfano
Siku 4:
hakuna upungufu wa kipimo cha nasaba ambacho kinaweza kutuambia kuhusu familia yetu na muundo wa vinasaba. Zinathibitisha ukweli: upende au usipende, sifa zote za kimwili zinatokana na wazazi wetu. Na, kadri tunavyozeeka, ndiyo tunavyotambua kwamba tabia zetu nyingi zinatoka kwao.
Labda unapenda hili. Labda inatuudhi kidogo. Labda inakuvuruga kabisa.
Labda kitu pekee unachotaka ni damu ya asili ya familia yako kutembea kwenye mishipa yako.
Maandiko yanazungumza kuhusu miti ya familia zetu kwa njia ambayo inaonekana ni nzuri zaidi- mti wa familia ya milele. Yohana 1:12 inatuambia kwamba Yesu anatoa haki ya kuwa wana wa Mungu kwa wale waliaminio jina lake. Anatupa mti mpya wa familia, na nafasi ya kuzaliwa na Mungu, tukiwa hai na vinasaba vya kiroho vipya. Alitimizaje kazi hii? Kwa mti mwingine--Msalaba.
Yesu alikuja ili afe, kama sadaka. Alichukua nafasi yetu. Mwana wa Mungu asiye na dhambi alibeba dhambi zetu na kufa kwa niaba yetu ili tuwe wana wa aliye juu. Mwana halisi wa Mungu aliachwa na kukataliwa, ili kwamba wewe na mimi tusiachwe na kukataliwa. Hatutaachwa, kwa sababu Yesu aliachwa kwa ajili yetu.
Kwa kifo chake msalabani, Yesu alituingiza kwenye familia mpya-- familia ya Mungu. Kwa kufufuka kwake, alinyang'anya mauti nguvu juu ya wote walio wa familia yake. Katika familia yake, wote tunaishi katika mfereji wa baraka za Baba. Kama wana wake, tunaishi katika ukweli huu!
• Hatutaweza kushinda uangalizi wa Mungu.
• Hatutaweza kumaliza upendo wa Mungu.
• Hatutaweza kwenda Mungu asipofika.
• Hatutaweza kuponyoka vidoleni mwake.
• Kila siku tutaamka katika rehema mpya za Mungu.
• Mungu atakutana na mahitaji yetu yote.
Katika Kristo, umechaguliwa, unapendwa, unathaminiwa, unatakiwa, na unaaminiwa na Mungu--Baba yako halisi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha - kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake.
More