Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano
Sasa Tenda
Usimalize Mpango huu wa Biblia bila kufanya kitu kuihusu. Viongozi wanatekeleza kulingana na taarifa na inaleta mabadiliko. Utachukua hatua ipi? Mungu yu tayari kutenda zaidi ya unavyoweza kuuliza, kufikiria, ama kuwaza, kupitia nguvu yake ambayo i kazini.
- Nidhamu ya Kuanza: Ukijua wewe ni nani, ama ni nani unataka kuwa, utajua matendo unayofaa kufanya. Kulingana na mtu ungependa kuwa, unahitaji kuanza nidhamu ipi?
- Ujasiri wa Kuacha: Kulingana na mtu ungependa kuwa, unahitaji ujasiri wa kuacha nini? Usifikirie tu mambo mabaya. Labda unahitaji kuacha kitu muhimu na kukipa kwa mtu mwingine.
- Mtu wa Kumwezesha: Utamwezesha nani? Usiwe kifuniko cha wale unaowaongoza. Pengine hata utamwezesha mtu kufanya kitu muhimu ambacho ulikuwa na ujasiri wa kuacha.
- Mfumo wa Kuumba: Ni wapi unaona mivutano? Pana shida wapi katika shirika? Ni mfumo upi unahitaji kuumba ili kupata matokeo ambayo unataka?
- Uhusiano wa Kuanzilisha: Kulingana na mtu ungependa kuwa, unahitaji kukutana na nani? Ni uhusiano upi unahitaji kuanzilisha? Unaweza kuwa uhusiano mmoja kutoka kubadilisha maisha yako.
- Hatari Unayohitaji Kuchukua: Kulingana na mtu ambaye ungependa kuwa na yale ambayo ungependa kufanya, ni hatari ipi unayohitaji kuchukua? Ikiwa daima utangojea mpaka uko tayari, kamwe utachelewa.
Mwishowe, kuwa mtu ambaye Mungu alikuumba uwe. Watu wanafuata kiongozi aliye mkweli kuliko kiongozi ambaye daima ni sahihi.
Nena na Mungu: Mungu, ninaamini ya kwamba utafanya zaidi kuliko ninavyoweza kufanya kwa nguvu yangu mwenyewe. Utanipa hekima, ujasiri, na nguvu kuchukua hatua ifuatayo?
Kuhusu Mpango huu
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.
More