Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano

Six Steps To Your Best Leadership

SIKU 4 YA 7

Mfumo wa Kuumba

Fikiria kuhusu shida kazini, ama katika kikundi chako, nyumbani mwako, ama maishani mwako inayoendelea kurejea. Pengine unafikiri kwamba shida ni katika kudhibiti ubora, huduma kwa wateja, watu wasiofaa, ama nyumba shaghalabaghala, lakini huenda shida ni mifumo.

Kama viongozi, tunapenda kuwalaumu watendakazi ilhali shida ni mifumo ya wakuu. 

Pengine unafikiri, “hatuna mifumo,” ama “tunatumia uhusiano; hatuhitaji mifumo.” Kwa heshima, una mifumo. Pengine mfumo wako ni kuanza siku kwa kuangalia baruapepe, kutatua shida ukizifikia, na kurudi nyumbani ukiwa umefadhaika. Hata hivyo, huo ni mfumo.

Una mifumo kwa kusudia ama bila kupanga, lakini vyovyote vile, unayo mifumo. Na mifumo unayo ni matokeo ya yale uliyoumba ama kustahimili. Kwa hivyo, ukitaka matokeo bora zaidi, anza kwa kuumba mfumo bora zaidi. 

Katika mlango wa kwanza wa Biblia, dunia ilikuwa haina umbo, na Mungu akasema, “iwepo nuru.” Kisha akaendelea kutenganisha nuru na giza, nchi na anga, ardhi na maji, ndege na samaki, na kadhalika. Pengine utagundua kwamba Mungu anashughulikia mifumo maalum pamoja na haachi mpaka anakiri kwamba ni mwema. Hatimaye, Mungu aliumba wanadamu na kuwapa maagizo ya utunzaji wa yote yaliyoumbwa— pamoja na mfumo wa kupumzika siku moja katika kila wiki. 

Uumbaji ulianza kwa mfumo. Mtume Paulo anaiita Kanisa mwili mmoja ulio na sehemu nyingi zote zikifanya kazi zikilenga nia muhimu. Huo ni mfumo. Mfumo ulio na kiongozi bora zaidi—Yesu. 

Kama ulimwengu, kama kanisa, kama mwili wako, maisha yako imejaa mifumo. Mifumo yenye afya haitokei kwa bahati. Inaumbwa kimakusudi. 

Unahitaji kuumba mfumo upi ili upate matokeo unayotaka? 

Waza: Nimempa Yesu uongozi wa mfumo wangu mkuu—maisha yangu? Nina mivutano ipi, na ni mifumo ipi itakayoitatua?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Six Steps To Your Best Leadership

U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.

More

Tungependa kushukuru Craig Groeschel na Life.Church kwa ajili ya kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.craiggroeschel.com/