Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano
Mtu wa Kumwezesha
Mmojawapo wa vitu vya kwanza ambavyo Yesu alifanya katika miaka yake mitatu ya utumishi kwa umma duniani ulikuwa kutafuta watu wa kuwawezesha. Alipata 12, lakini labda uanze na mmoja kwa sababu wewe si Yesu.
Ikiwa hutawawezesha wengine, ninakuahidi—itafunika kazi yako. Kazi yako haifaulu kwa ufanyacho; inafaulu kwa wale unaowawezesha.
Ikiwa Yesu, Mwana wa Mungu, alitegemea watu ili vitu vitendeke, inaelekea kwamba hatutajenga kitu kikuu peke yetu. Jenga watu na pamoja mtajenga kitu kikuu.
Jana tulizungumza kuhusu kuwa na ujasiri wa kuacha. Pengine utahitaji kuacha shughuli muhimu unazopenda kufanya. Ikiwa una ripoti, zoezi, ama mradi, tafakari kuyagawa majukumu. Ikiwa mtu anaweza kufanya kitu kwa ubora nusu wa wako lakini ana uwezekano wa kukua, gawa majukumu na utaona atakua.
Yesu alianza kwa kutafuta watu wa kuwawezesha na alitamatisha kazi yake duniani kwa kugawa mmojawapo wa majukumu yake muhimu kwa wafuasi wake wote. Tunaliita Agizo Kuu, na nilipoangalia, inafanya kazi.
Unaweza kupeana nini? Utampa nani? Utawaendeleza na kuwafunza vipi?
Ukiwawezesha watu sahihi, watahisi kana kwamba wanathamaniwa, watakua kama viongozi, utaweza kulenga kwingineko, na chochote unachoongoza kitajengeka.
Unaweza kudhibiti kazi yako, ama ukuzi, lakini huwezi kuwa na zote mbili. Utawezesha nani?
Nena na Mungu: Mungu, asante kwa kuniamini kuongoza baadhi ya watu wako. Ninafaa kumwezesha nani? Ninafaa kumwezesha kufanya nini?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.
More