Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano

Six Steps To Your Best Leadership

SIKU 1 YA 7

Nidhamu ya Kuanza

Mke wangu Amy, watoto wangu, na wafanyakazi wangu wangekuambia kwamba kujenga viongozi si kitu tu ambacho ninapenda kufanya, ni sehemu kuu ya uzima wangu. Ninaamini ya kwamba kiongozi akiimarika, kila mtu anaimarika.

Tafakari swali hili: “Kuongoza watu ni jambo tu ambalo ninataka kufanya, ama ni sehemu ya uzima wangu”?

Jibu lako ni muhimu kwa sababu viongozi wengi wanajaza mipango yao ya maendeleo na malengo ya kutenda: “Ninataka kufanya zaidi na watoto wangu, nitamtendea mke wangu vitendo vya hisani bila utaratibu, nitafanya zaidi kuwawezesha watu ambao ninawaongoza.” Hata hivyo, viongozi maarufu zaidi wana malengo ya kuwa: “Nitakuwa mama mwenye subira anayependa kwa dhati, nitakuwa mume anayetegemeza mke wangu na kumpenda vyema, nitakuwa msimamizi anayeongoza kwa mfano.” 

Viongozi maarufu wanaanza na kuwa kisha kutenda kinatitirika kutoka hapo.

Hata tukitumia vipimo vya kidunia, Yesu anasemekana kuwa kiongozi maarufu zaidi kamwe. Alifanya kazi hadharani kwa miaka mitatu pekee ilhali katika wakati huo akapata maelfu wa wafuasi. Karne mbili baadaye, kitabu ambacho kimeuzwa zaidi kinasimulia kisa cha maisha yake, na mabilioni za watu kutoka pande zote za dunia wametoa maisha yao yote kumfuata.

Mara saba katika kitabu cha Yohana, Yesu alitangaza matamko yenye nguvu ya kuwa . Ukiyasoma leo, utaona kwamba kila tamko kinaafikiana na alichotenda na anachoendelea kufanya katika ulimwengu wetu.

Unapojua kuwa kwako yaani wewe ni nani, utajua cha kutenda. Hususan, pengine utajiuliza, “mtu ambaye ningependa kuwa angefanya nini?”  Katika chochote ambacho unachagua kufanya, ninapendekeza kwamba uanze kwa mambo madogo. Nidhamu ndogo zikifanywa mara kwa mara zinaleta matokeo makubwa hatimaye. 

Ikiwa ungependa kuwa kiongozi anayejali, labda utaandika noti moja kila siku ya kumhimiza mtu. Ikiwa ungependa kuwa mtu nadhifu, pengine anza na kutandika kitanda chako. Ikiwa ungependa kuwa kiongozi anayefuata moyo wa Mungu, inaelekea kwamba utaanza na kunena na yeye kila asubuhi. Tenda kile ambacho kinakuongoza kuwa kiongozi ambaye ungependa.

Nena na Mungu: Mungu, uliniumba; unanijua. Utanipa maneno kujua mimi ni nani na nguvu kujua ninachofaa kutenda?

Sikiliza tangazo langu la uongozi kwa mafunzo zaidi

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Six Steps To Your Best Leadership

U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.

More

Tungependa kushukuru Craig Groeschel na Life.Church kwa ajili ya kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.craiggroeschel.com/