Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano
Ujasiri wa Kuacha
Ikiwa kulikuwa na mtu aliyezaliwa na uwezo wa uongozi bora zaidi kutoka Mungu, ilikuwa Samsoni, lakini maisha yake yaliangamia kabisa kwa sababu hakuwa na ujasiri wa kuacha.
Mambo yakaanza kumharibikia katika Waamuzi 16:1 NEN: Siku moja Samsoni alienda Gaza, akamwona mwanamke kahaba.
Gaza ni kilomita 40 kutoka kijiji cha Samsoni cha Zora. Gaza ilikuwa jiji kuu la Wafilisti ambapo Samsoni alikuwa Adui Mkuu wa Umma. Aidha, Samsoni alipoishi—hapakuwa na Uber. Samsoni alitembea kilomita 40 katika nchi ya adui zake ili kumwona kahaba.
Hizo ni hatua 56,250. Samsoni hakuharibu maisha yake mara moja. Alichukua hatua 56,250 akifuata mwelekeo mbaya.
Si tofauti katika vikundi vyetu, mashirika yetu, kazi zetu, afya yetu, na familia zetu. Hatuazimii kuziharibu mara moja. Hayo huwa yanafanyika uamuzi mmoja mbaya, hatua mmoja mbaya, tabia mmoja mbaya, siku moja baada ya siku.
Kwa hivyo twahitaji nini? Ujasiri wa kuacha. Kusema la. Kupunguza unachofanya. Kukataa kuchukua hatua nyingine kuelekea mwelekeo mbaya. Unahitaji kuacha nini?
Hii haihusu kuacha yaliyo mabaya pekee. Wewe ni msimamizi? Labda kuna mkutano wastani ambao unaweza kuacha. Ikiwa unatumia raslimali katika miradi ya wastani, hutapata matokeo makuu. Ni miradi ipi unahitaji kuacha? Ni shughuli zipi zitafaa kuachwa ili ukue kama kiongozi? Kupata matokeo zaidi kama kiongozi, pengine unahitaji kupunguza ufanyacho.
Labda haihusu kazi. Pengine wewe ni kama Samsoni, na umechukua hatua mmoja, mbili, ama pengine 2,000 ukifuata mwelekeo mbaya katika uhusiano, tabia, ama afya yako. Jibu ni lilelile—hujachelewa kuwa na ujasiri wa kuacha.
Waza: Nikifikiri ningependa kuwa nani, ni nini ambayo ninafaa kuwa na ujasiri wa kuacha? Ni nini inachochea matokeo mabaya? Ni hisia zipi ama mahali ambazo zinaniingiza matatani? Nani anaweza kunisaidia kuacha?
Kuhusu Mpango huu
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.
More