Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

SIKU 8 YA 9

“Mfalme Aliyesulubiwa”

Kuhani mkuu alipomwuliza, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu?” Yesu akasema, “Mimi ndiye.” Kwa kujibu hivyo, Yesu anasema: “Nitakuja duniani na utukufu wenyewe wa Mungu na kuhukumu ulimwengu wote.” Ni tamko la kushangaza. Anadai umungu.

Kutoka vitu vyote ambavyo Yesu angesema—na kuna maandiko mengi, mada, picha, istiari, na vifungu vya Maandiko ya Kiebrania ambayo angetumia kutuambia yeye ni nani—lakini maneno yake maalum ni kwamba yeye ni hakimu. Kwa chaguo lake la andiko, Yesu anatulazimisha tuone kinaya. Kuna mvurugo kuu. Hakimu wa dunia nzima, anahukumiwa na ulimwengu. Anafaa kuketi katika kiti cha hukumu, na tunafaa kuwa kizimbani, tumefungwa minyororo. Kila kitu kimegeuzwa na juu i chini.

Punde tu Yesu anadai kwamba yeye ni hakimu huyu, punde tu anadai umungu, jibu ni mlipuko. Marko anaandika:

Yesu akasema “Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni.” Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi?” “Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi?” Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa. Wengine wakaanza kumtemea mate; wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, “Tabiri!” Hata watumishi nao wakampiga makofi.
(Marko 14:62–65)

Kuhani mkuu anararua nguo zake, ishara ya hasira kuu zaidi, hofu, na huzuni. Kisha kesi yote inazorota. Hakika si kesi tena; ni fujo. Baraza la waamuzi na majaji wanaanza kumtemea na kumchapa. Katikati ya kesi, wanarukwa akili. Papo hapo anapatikana na hatia ya kufuru na kuhukumiwa kwamba anastahili kifo.

Ingawa mimi nawe hatuwezi kumtemea Yesu uso, bado tunaweza kumkejeli na kumkana. Ni katika njia zipi ambazo tuna tabia ya kutokubali Yesu kama Mungu?

Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller
kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller

Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.
siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea ufahamu mpya kuhusu uhusiano kati ya maisha yetu na maisha ya mwana wa Mungu, tunapoelekea msimu wa Pasaka. Sasa hivi, JESUS THE KING ni kitabu na mwongozo wa mafundisho kwa vikundi vidogo, kinachopatikana mahali popote vitabu vinauzwa.

More

Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide