Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano
“Kifo cha Kifo”
Yesu aliwaambia wafuasi wake, “Nitafufuka tena siku ya tatu.” Alisema hivi katika Marko 8, tena katika Marko 9, na tena katika Marko 10.
Ukikumbuka jinsi ambavyo Yesu alijirudia, jambo hili linahitaji udadisi zaidi. Siku ya tatu baada ya kifo cha Yesu, hakuna wafuasi wa kiume; wafuasi wake wa kike wapo, lakini wanaleta viungo na marashi vya thamani kuu vinavyotumiwa kupaka maiti kidesturi. Hakuna anayetarajia ufufuo. Ikiwa ungekuwa mwandishi wa Injili Marko, unajaribu kuandika kisa cha ubunifu kinachoweza kuaminika, na ulikuwa na Yesu akjiirudia kwa wafuasi wake kwamba atafufuka siku ya tatu, hungemfanya hata mfuasi mmoja afikiri baada ya kifo cha Yesu na kusema kwa wenzake, “Aisee, ni siku ya tatu. Pengine tuende tuangalie kaburi la Yesu. Itamwathiri nani?” Tungeelewa. Lakini hakuna mtu aliyesema hivyo. Hakika, hawakutarajia ufufuo hata kidogo. Hawakuufikiria. Malaika aliyesimama mbele ya kaburi tupu alilazimika kuwakumbusha wanawake: “Mtamwona, kama alivyowaambia.” Ikiwa Marko angekuwa amebuni kisa hiki, hangekiandika katika namna hii.
Na hii ndio hoja kuu: Ufufuo ulikuwa jambo ambalo wafuasi wa kwanza hawakuweza kuelewa, na vigumu kwa kuamini, kama vile ni vigumu kwa wengi wetu leo kuamini. Naam, sababu zao zingekuwa tofauti na zetu. Wagiriki hawakuamini ufufuo; mtazamo wa Wagiriki ilikuwa kwamba maisha ya baadaye yalikuwa roho kuachishwa huru kutokana na mwili. Kwao ufufuo haungekuwa sehemu ya maisha baada ya kifo. Nao Wayahudi, wengine waliamini ufufuo wa kila mtu baadaye ambapo ulimwengu wote ungefanywa upya, lakini hawakuwa na dhana ya mtu mmoja kufufuka kutoka mautini. Watu walioshi katika siku za Yesu hawakuwa na uzoefu wa imani ya ufufuo vile vile kama sisi.
Je, ni vigumu kwako kuamini kwamba Yesu alifufuka kutoka mautini? Ufufuo wa Yesu unakupa matumaini vipi?
Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller
kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller
Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea ufahamu mpya kuhusu uhusiano kati ya maisha yetu na maisha ya mwana wa Mungu, tunapoelekea msimu wa Pasaka. Sasa hivi, JESUS THE KING ni kitabu na mwongozo wa mafundisho kwa vikundi vidogo, kinachopatikana mahali popote vitabu vinauzwa.
More
Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide