Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano
“Ilimpasa Yesu Afe”
Kwa kutumia neno ilimpasa, Yesu anaashiria kwamba anapanga kufa—kwamba tendo hilo ni kwa hiari. Hatabiri tu kwamba itatendeka. Pengine hili ndilo linalokera Petro zaidi. Ni jambo moja kwa Yesu kusema, “Nitapigana na nitashindwa,” na jingine kusema, “Hii ndiyo sabau nilikuja; ninadhamiria kufa!” Petro haelewi kabisa.
Ndio maana punde Yesu anasema hivi, Petro anaanza 'kumkemea'. Kitenzi hiki kimetumika kwingine kuashiria anachofanyia Yesu mapepo. Hii inamaanisha kwamba Petro anamhukumu Yesu kwa maneno makali zaidi. Mbona Petro ni mpotevu mno, hadi anamgeukia Yesu punde tu baada ya kumtambua kuwa Masihi? Kutoka utotoni Petro alikuwa ameambiwa kwamba Masihi alipokuja atashinda maovu na dhuluma kwa kutawala katika kiti cha enzi. Lakini hapa Yesu anasema, “Ndio, mimi ni Masihi, Mfalme, lakini sikuja kuishi bali kufa. Sipo hapa kuchukua nguvu bali kuipoteza; nipo hapa kutumika wala si kutawala. Vivyo hivyo ndivyo nitakavyoshinda maovu na kurekebesha vyote.”
Yesu hakusema tu kwamba Mwana wa Adamu atateseka; alisema kwamba ilimpasa Mwana wa Adamu ateseke. Neno hilo ni muhimu sana hadi linatumiwa mara mbili: “imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi na . . . imempasa kuuawa.” Neno hilo linabadili na kudhibiti sentensi kamili, na maana ni kwamba kila kitu katika orodha hii ni la lazima. Sharti Yesu ateseke, sharti akataliwe, sharti auawe, sharti afufuliwe. Hili ni neno la maana kuu katika kisa cha dunia, na ni neno linalotisha. Yesu hasemi tu kwamba “nimekuja kufa” bali anasema “inanipasa nife. Ni sharti nife. Ulimwengu hauwezi kufanywa upya, wala maisha yako, nisipokufa.” Mbona ni sharti Yesu afe?
Ilikuwa vigumu kwa Petro kuelewa umuhimu wa kifo cha Yesu. Mbona ni vigumu kwake—na kwetu—kukubali?
Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller
kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller
Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea ufahamu mpya kuhusu uhusiano kati ya maisha yetu na maisha ya mwana wa Mungu, tunapoelekea msimu wa Pasaka. Sasa hivi, JESUS THE KING ni kitabu na mwongozo wa mafundisho kwa vikundi vidogo, kinachopatikana mahali popote vitabu vinauzwa.
More
Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide