Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano
"Kuitwa na Mfalme"
Injili si ushauri: Ni habari njema kuwa hauhitaji kupata njia yako kwa Mungu; Yesu tayari amekutendea. Na ni zawadi unayopokea kupitia neema pekee—kupitia kibali usichostahili kabisa kupata kutoka kwa Mungu. Ukikamata zawadi hiyo na uendelee kuishikilia, basi wito wa Yesu hautakuvuta katika ushabiki au uwastani. Utakuwa na hamu ya kumfanya Yesu kuwa lengo lako halisi na la kipaumbele, kumzunguka; ilhali ukikutana na mtu aliye na seti tofauti za vipaumbele, imani tofauti, hutadhani kuwa yeye ni duni kukuliko. Utataka kuwatumikia badala ya kuwakandamiza.
Mbona? Kwa sababu injili si tu kuchagua kufuata ushauri, bali ni wito wa kumfuata Mfalme. Si tu mtu aliye na uwezo na mamlaka ya kukuambia kinachohitajika kufanywa—lakini mtu mwenye uwezo na mamlaka ya kufanya kinachohitajika kufanywa, kisha kukitoa kwako kama habari njema.
Tunaona wapi aina hii ya mamlaka? Ubatizo wa Yesu tayari uliambatana na ishara za kimiujiza ambazo zilitangaza mamlaka yake ya kimungu. Kisha tunaona Simoni, Andrea, Yakobo na Yohana wakimfuata Yesu bila kuchelewa—kwa hivyo wito wake wenyewe una mamlaka. Marko anaendelea kujenga mada hii:
"Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na Sabato ilipofika, Yesu alienda katika sinagogi na akaanza kufundisha. Watu walistaajabishwa na mafundisho yake, kwa sababu aliwafundisha kama aliyekuwa na mamlaka, sio kama walimu wa sheria."
(Marko 1:21–22)
Marko anatumia neno mamlaka kwa mara ya kwanza; neno hilo kihalisia linamaanisha “kutoka kwa mambo ya asili.” Asili yake ni sawa na neno mwandishi. Marko anamaanisha kuwa Yesu alifundisha kuhusu maisha kwa mamlaka ya kiasili wala si mamlaka yaliyotokana na wengine.
Maisha yako yangekuwaje kama ungeyasalimisha kwa huyu mfalme kamili? Maisha yako ya kikazi? Maisha yako ya kimapenzi? Maisha yako ya kifamilia? Maisha yako ya kifedha? Maisha yako ya kijamii?
Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller
kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller
Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea ufahamu mpya kuhusu uhusiano kati ya maisha yetu na maisha ya mwana wa Mungu, tunapoelekea msimu wa Pasaka. Sasa hivi, JESUS THE KING ni kitabu na mwongozo wa mafundisho kwa vikundi vidogo, kinachopatikana mahali popote vitabu vinauzwa.
More
Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide