Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

TabiaMfano

Habits

SIKU 6 YA 6

Ushindi Mdogo

Kama domino, kujenga na kuvunja tabia inajumuisha hatua nyingi zisizosemwa ambazo ni za kila siku na zinawezekana ili kupata badiliko kuu. Mchungaji Craig Groeschel alisema kwa ufupi: “Nidhamu ndogo zikifanywa kwa mfululzo zinaweza kuleta matokeo makubwa baada ya muda.” Yaani, ushindi mdogo ni muhimu.  

Tabia si mwisho wa safari ambayo utafikia siku moja—bali ni hatua ndogo unayochukua kila siku. Miongoni mwa ushindi mdogo kuna tabia muhimu ziitwazo tabia za jiwe la tao. Njia bora zaidi kuelewa tabia za jiwe la tao ni kujifunza maana ya jiwe la tao. Hili ni msamiati maalum ya wachoraji ramani za majengo ya jiwe ambalo lina umbo la kabari ambalo lingewkwa juu ya na kati ya tao la mawe au matofali. Kila jiwe katika tao kinasukuma jingine hadi jiwe la tao, na umbo lake la pembetatu linaliwezesha kuwa nguzo ya tao lote. 

Ukiondoa jiwe la tao, ujenzi wote utaanguka. Katika biolojia, spishi ambayo ni jiwe la tao ni aina ambayo mazingira yanaitegemea. Vile vile, tabia ya jiwe la tao ni nguzo na himizo ya tabia nyingine maishani mwako. 

Vitabu vingi kuhusu tabia vitakuambia kuhusu tabia za jiwe la tao, ifaavyo, lakini pengine havitakuambia kwamba kuna jiwe jingine. Yesu alijiita jiwe la pembeni ambalo ni jiwe ambalo pia ni nguzo ya ujenzi wote wa nyumba. Unaweza kufuzu katika tabia za jiwe la tao lakini bado mjengo wako uporomoke ikiwa msingi wako hauna Yesu kama jiwe la pembeni. 

Hapa pana orodha mfupi ya tabia za jiwe la tao ya kutafakari. Unaweza kuongeza zipi maishani mwako? Yesu ndiye jiwe la pembeni kwako?

  1. Amka mapema ili uanze siku yako na Yesu.
  2. Hakikisha umelala angalau saa nane kila usiku. 
  3. Kula angalau mlo mmoja kila siku na familia yako au marafiki wa karibu.
  4. Nenda kanisa kila wiki, na ushiriki kwa kutoa na kuhudumu huko. 
  5. Fanya mazoezi ya viungo vya mwili angalau mara tatu kwa wiki kwa dakika 20.
  6. Tangaza ukweli kujihusu kila siku. 

Kujenga tabia njema na kuvunja mabaya ni mchakato wa kila siku maishani mwako. Kifaa kifuatacho kitakusaidia unapomfanya Yesu awe jiwe la pembeni kwako. 

Utambulisho Bora

Omba Usaidizi

Jipe fadhili

Chunguza na Badilisha

Amini Mchakato Wa Mungu

Ushindi mdogo

Pata Mwongozo wa Tabia Njema ya Kila Siku. 

siku 5

Kuhusu Mpango huu

Habits

Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/