TabiaMfano
Jipe fadhili
Siku ambayo unaamua kuchukua utunzi wa tabia njema za kila siku kwa uzito ndiyo siku ambayo unatoka “eneo la ukamilifu.” Hii inahusiana na mada ya leo: Jipe fadhili. Katika siku ambayo hutawajibika na tabia njema uliyoamua kufanya, jipe fadhili.
Usijisalimishe kwa fikra hasi kujihusu na kujichukia. Shikilia ukweli wa Mungu na utambulisho bora Mungu anarejesha ndani yako. Chukua hii fursa kuchimbua tatizo kuu chini kidogo. Chukua muda kutafakari kuhusu utambulisho bora wako na kuomba usaidizi kutoka watu unaowaamini.
Labda umekosea. Ama pengine hujakosea. Vyovyote vile, uliza Mungu, na labda watu fulani, wakusamehe. Kisha, tumia fursa hii kukua, kupata uponyaji wa kina, na kama nafasi nyingine kusisitiza tabia njema ya kila siku ambayo itakabiliana na shida zozote zile. Kama vile ukishikwa na homa na kinga kinaimarishwa mwilini mwako, hii ni fursa ya kujidhibiti ambako Mungu alikupa kukue na kuimarishwe.
Yesu alituamuru tumpende Mungu kwa hali na mali na kupenda wenzetu kama tunavyojipenda. Hizi zinajulikana kama amri mbili kuu. Lakini kwa kweli, kuna ya tatu ambayo imefichika hapo. Kupenda wengine kama unavyojipenda, lazima ujipende! Kwa hivyo, hata kama ni kwa sababu Yesu alikuamuru tu, jipe fadhili ukikosea. Usikate tamaa. Usijichambue kupita kiasi. Simama tu, tazama juu, omba msamaha, na ujaribu tena!
Omba: Mungu twakushukuru kwa upendo wako ambao unanipa nguvu kufanya vyema na neema nikikosea. Ninahitaji usaidizi wako, na ninaamini ya kwamba utabaki nami hata nikikosea. Amina.
Kuhusu Mpango huu
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.
More