TabiaMfano
Utambulisho Bora
Sote tungependa tabia njema za kila siku. Lakini badala yake tunafanya vitu kama vile kuamka kwa kuchelewa, kuchelewa kazini, kuchelewa kurudi nyumbani, kuwapigia watoto wako kelele, kula ama kunywa “moja zaidi tu,” na kuangalia baruapepe zetu kitandani.
Kwa hivyo, tutaanza aje kuwacha tabia mbaya na kutengeneza nzuri? Hakuna mpango wa rahisi wa hatua tatu ambao utaniweka huru? La hasha. Lakini kuna tumaini, na neno la Mungu limejaa tumaini.
Mchungaji wa Life.Church, Craig Groeschel, anasema kwamba sababu moja kuu ya watu kukosa kuwa na tabia njema na kukosa kuvunja tabia mbaya ni kwamba utambulisho wetu umepotoka kwa hivyo unazuia kufanikiwa kwetu. Hii ndiyo njia ya kwanza tutatumia kugundua njia bora kuunda na kuvunja tabia: utambulisho bora.
Mara nyingi wakati ambapo tuko tayari kuanza kitu upya ama kuvunja tabia mbaya, tunaunda mpango ambao una msingi wa yale ambayo tutatenda. Badala yake tunafaa kuanza malengo na msingi wa Mungu ni nani na ni nani ambaye tunataka kuwa. Kusema, “Nitakimbia marathoni,” kuna msingi wa yale ambayo unataka kutenda. Kusema, “Nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha, na kwa nguvu yake Mungu ningependa kuwa mkimbiaji,” kuna msingi wa Mungu ni nani na ni nani unatamani kuwa. Hili ni lengo lenye msingi wa utambulisho. Tunafaa kuweka nani kabla ya kutenda.
Malengo yaliyo na msingi wa utambulisho ni sehemu moja ya utambulisho bora. Kipengele kingine cha uhuru kinatokana na kuchimbua machungu yaliyopita, uongo ulioamini, kutosamehe, makosa, na hali ya maisha ambayo ilikufanya uamini sura ya maisha yako ambayo Mungu hakukuumba uwe. Unapogundua uongo, utataka kuubadilisha na ukweli wa Mungu unaotoka Neno lake. Utambulisho bora ambao una msingi wa yale ambayo Mungu anasema kukuhusu ni msingi wa kuvunja tabia mbaya na kuunda njema.
Kwa mfano, wengi wetu wameamini uongo kama vile, “Nitakuwa hivi milele.” Huu ni woga unaotokana na utambulisho na unahitaji ukweli unaotokana na utambulisho kama vile, “Roho wa Mungu hakunipa woga. Alinipa nguvu, upendo, na uwezo wa kujidhibiti!”Ni uongo upi unaotokana na utambulisho wako ambao unaweza kubadilisha na ukweli wa Mungu?
Omba: Mungu, ni tabia zipi ambazo ninafaa kuwacha? Ni sehemu zipi za kindani za utambulisho wangu ambazo pengine zinanifanya niwe na tabia hizo? Roho Mtakatifu, nahitaji nguvu yake kufanya mabadiliko haya. Amina!
Kuhusu Mpango huu
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.
More