TabiaMfano
Omba Usaidizi
Jana tulizungumza kuhusu kupata utambulisho bora katika ukweli wa Mungu kukuhusu. Pengine somo la leo ndiyo muhimu zaidi, kwani ni muhimu kwa masomo mengine: omba usaidizi.
Katika kitabu cha Waebrania—ambacho ni barua kwa Wayahudi ambao walikuwa wakimfuata Yesu—imedokezwa kwamba kukosa kukutana na waumini wengine si ukosefu tu wa tabia njema, bali ni uwepo wa tabia mbaya.
Neno asilia la Kigiriki la “tabia” katika Waebrania 10:24-25 ni éthos ambacho kina maana ya kitu ambacho kimekuwa desturi, ambacho pengine kimeagizwa na sheria au nyinginezo. Tabia daima ni dawa ya kitu. Tabia njema, kama vile kujiunga na jamii ya kidini, ni dawa nzuri. Tabia mbaya, kama vile kujitenga tunapopambana, ni dawa ya uchungu na utamaushi zaidi.
Kwa mfano, utahitaji mada ya leo (omba usaidizi) ili kupiga hatua na mada ya jana: utambulisho bora. Mapambano mengi yaliyofichika na ya kindani yatadhihirika pekee tunapozungumza na watu ambao tunawaamini, washauri, wachungaji, wake/waume, na Mungu ambaye tunamwamini.
Umeifanya desturi kukosa kuwa katika jamii na wengine? Ni sawa. Dawa ni rahisi: omba usaidizi. Lakini usiombe usaidizi mara moja tu. Ifanye iwe desturi kukutana kwa kawaida kujumuika pamoja waziwazi na watu wengine ambao wanamfuata Yesu Kristo.
Jiulize: Nitaongea na nani kuhusu tabia ambazo ninaharibu kuunda na kuvunja? Nitawaambia nini? Nitaongea lini na wao?
Kuhusu Mpango huu
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.
More