Soma Biblia Kila Siku 1Mfano
Wasamaria walivutwa kumkaribisha Yesu mjini kwao kutokana na ushuhuda wa yule mwanamke Msamaria aliyekutana na Yesu kisimani. Nao walipomsikiliza Yesu wakamwamini na kushuhudia kuwa hakika Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu (m.39-41). Je, wewe pia unamwamini Bwana Yesu? Basi msuhudie kwa neno na tendo. Pengine unafikiri utaanza baadaye, baada ya kujua zaidi jinsi ya kufanya? Basi soma tena m.35 na kuzingatia maana yake! Ni sasa Yesu yupo tayari kukutumia kuleta wokovu kwa wengine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz