Jinsi ya Kujifunza Biblia (Misingi)Mfano
Usomaji Bora wa Biblia Hubadilisha
Wale walio tayari kuwa kwenye mazingira magumu hutembea kwenye siri. – Theodore Roethke
Hebu fikiria unaingia ofisini kwa daktari kwa sababu unajisikia unaumwa lakini badala ya kutumia kipima joto kama inavyotakiwa kuwa (kwa kuweka mdomoni, sikioni, au kwenye paji la uso wako), kinawekwa mkononi. Ndipo baada ya sekunde chache, muuguzi anakichukua na kukwambia joto lako liko sawa.
Utafanyaje? Ni kweli inaonekana sawa, lakini hukukitumia katika njia sahihi.
Kwa utaratibu huo, kimetumika kwa njia hiyo, cha muhimu kwamba kipima joto kilipima joto la mle ofisini. Si kwamba kipima joto chenyewe kilikuwa kimeharibika au kuvunjika. Bali hakikutumika sawa sawa.
Vivyo hivyo, tunapoiweka Biblia mbali nasi tunakosa ile nguvu, kweli, na maisha yanayotakiwa kufikiwaa. Biblia ni moja ya msingi ambayo Mungu anataka kujifunua kwetu. Kama tunataka, kuwa, na kufanya kila kitu Mungu alichokusudia huanza na kuianza Biblia na nyezo sahihi na kusudi.
Kwa maisha yangu ya kikristo, hizi ni nguzo saba bora ( zenye mabadiliko) za kujifunza Biblia:
- Kuelewa muktadha.
- Jenga tabia.
- Jizoeze kukariri.
- Kutumia nyezo sahihi.
- Kujifunza kwenye jamii.
- Kujumuisha maombi.
- Kutafuta mazingira magumu.
Mwenendo wako unaweza kujumuisha zaidi ya hayo, lakini si pungufu ya hayo saba. Yamenisaidia sana kukua zaidi ya vile nilivyofikiria inawezekana na naamini yanaweza kukusaidia na wewe pia.
Ninatumaini na ninaomba kwamba ujifunze kupenda neno la Mungu kwa shauku kubwa. Na mwishowe, kwamba hakika itakuwa taa ya miguu yako na mwanga kwenye njia yako.
Kuhusu Mpango huu
Ni rahisi kuhisi kwamba umeelemewa, huna vifaa vifaavyo, na kwamba umepotea inapokuja kwenye Neno la Mungu. Lengo langu ni kurahisisha mchakato huu wa kujifunza Biblia kwa kukufundisha kanuni tatu za muhimu katika kujifunza Biblia. Jiunge leo na mpango huu na utagundua namna ya kusoma Biblia si kwa taarifa pekee, bali pia kubadilisha maisha yako!
More