Jinsi ya Kujifunza Biblia (Misingi)Mfano
Usomaji Mzuri wa Biblia Unasaidiwa na Nyenzo
Mtu anakuwa mzuri kama nyezo zake zilivyo. – Emmert Wolf
Moja ya vitu navyovipenda kufanya siku napokuwa sipo kazini ni kukaa chini na kikombe chenye chai ya tangawizi-limao na kutazama maonesho ya mapishi. Inafurahisha kumuona Mpishi mkuu akiwa kazini. Kila wanachokifanya kina kuwa na kusudi kuanzia kwenye viungo wanavyotumia, joto wanaloliweka, mpaka kwenye vyombo wanavyovitumia kwenye ubunifu wao.
Kama ukiwauliza hawa wapishi wa ngazi ya kimataifa kwamba ni kitu gani cha muhimu katika mapishi yao, 99% watakupa jibu hilo hilo: viungo. Jinsi unavyokuwa na viungo vipya au adimu, ndivyo chakula kinavyokuwa kizuri zaidi.
Kwa wanafunzi wa Biblia, viungo vyetu ni nyenzo tunazotumia kutusaidia kuelewa maandiko. Kama tukitumia nyenzo nzuri, tutajenga uelewa mzuri wa ulimwengu wa Biblia na kujifunza jinsi ya kutumia ukweli tuliojifunza ndani ya neno la Mungu. Lakini tukiwa na nyenzo hafifu au "viungo" visivyo sahihi, uelewa wetu wa Biblia utakuwa na mapungufu na yawezekana kutuongoza katika njia hatari.
2 Timotheo inatutaka kuwa watenda kazi wanaoweza "kwa usahihi" kushika "neno la kweli." Njia bora unayojua kufanya hilo ni hii:
- Gundua nyenzo zilizopo za kukusaidia wewe kuielewa Biblia.
- Muombe Mungu akuongoze kwa mshauri mzuri wa kimungu akusaidie kutumia nyenzo.
Sasa, inaweza kuwa rahisi kupumbazwa na idadi ya nyenzo zilizopo. Kuna maoni, Kamusi, maana za maneno mbali mbali, ramani, mifumo ya lugha, na zaidi. Nyenzo namba 1 ambayo namshauri mwanafunzi wangu kuanza nayo ni rahisi: tafsiri nzuri.
Shukrani, nyenzo kama app ya Biblia ya YouVersion ni rahisi kufikia tafsiri nyingi za kukusaidia. Hapo ndipo napokutia moyo kuanzia.
Kuna hazina kwenye Neno la Mungu zikisubiri wale walio tayari kuzitafuta.
Dondoo: Unataka masomo yako ya Biblia kufikia katika viwango vya juu lakini huna uhakika uanzie wapi? Chagua mstari wako mmoja unaoupenda na uandike tafsiri 5 tofauti za mstari huo katika karatasi. Kuna tofauti au mfanano gani unauona? Umakini wako kama msomaji ni nyenzo mojawapo bora iliyopo.
Kuhusu Mpango huu
Ni rahisi kuhisi kwamba umeelemewa, huna vifaa vifaavyo, na kwamba umepotea inapokuja kwenye Neno la Mungu. Lengo langu ni kurahisisha mchakato huu wa kujifunza Biblia kwa kukufundisha kanuni tatu za muhimu katika kujifunza Biblia. Jiunge leo na mpango huu na utagundua namna ya kusoma Biblia si kwa taarifa pekee, bali pia kubadilisha maisha yako!
More