Jinsi ya Kujifunza Biblia (Misingi)Mfano
Usomaji Bora wa Biblia Unahifadhiwa na Maombi
Kuwa mkristo pasipo maombi ni kama kuwa na uhai pasipo kupumua. – Martin Luther
Moja ya chakula ninachokipenda ni kuku aliyeokwa mwenye viungo. Majira ya kiangazi kilichopita, nilitafuta jinsi ya kuweka viungo kwa sababu nilitaka kujifunza kitu gani kinatokea kwenye chakula kukifanya kitamu. Hiki ndicho nilichogundua.
Chakula kinapowekwa viungo, hasa jamii ya protini kama kuku, unafunika kwenye majimaji ya tindikali (kama siki au limao). Maji ya tindikali huvunja vunja ngozi ya nje ya nyama ili kwamba viungo viweze kuingia ndani zaidi.
Kuweka viungo huchukua muda. Huwezi kuweka kuku tuu kwenye viungo kwa dakika chache na ukategemea viungo kuingia ndani. Ni lazima utoe muda wa kutosha ili hatua ya viungo kuingia iweze kukamilika.
Maombi ni viungo kwa mkristo. Kuomba katika Biblia kunaturuhusu kukaa katika kweli ya Mungu kwa muda mrefu kiasi kwamba yataruhusu kuvunjika kwa vikwazo vya nje na "kututia" utamu zaidi ya vile ambavyo tusingeweza kuwa sisi wenyewe.
Tukiwa na ufahamu huo akilini mwetu, ngoja nishiriki nanyi ombi naloomba kila mara naposhika Biblia:
Bwana, tafadhali fungua neno lako, na fungua neno lako kwangu.
Hii inatayarisha nafasi akilini na moyoni mwangu kwa kitu kitakachotokea katika tabia za kila siku. Nataka kubadilishwa. Nataka Roho Mtakatifu kuniangazia neno. Na ninafanya makusudi haya wazi kwa kutamka ombi hili fupi.
Kuna (kwa uhakika) njia nyingi za kuunganisha ombi na muda wako wa Biblia. Kwa sasa, nakutia moyo kujaribu ombi hili fupi na uone mabadiliko gani yatatokea.
Dondoo: Je, unajikuta umechanganyikiwa katika maombi kwa sababu hujisikii kama Mungu anasikia au anakujibu? Ngoja nikupe ushauri ambao mchungaji wangu alinipa: shusha kiwango chako. Watu wengi wanadhani kusikia kutoka kwa mungu ni kwa miujiza, tukio la kubadilisha maisha. Kusema ukweli, Mungu na Roho Mtakatifu wanazungumza na wewe siku zote (hata mara kadha kwa siku!). Kushusha kiwango chako maana yake (1) kutarajia Mungu atasema nawe na (2) kwa makini kuangalia njia ndogo ambayo Mungu hufanya. Huhitaji kuona kichaka kinawaka kumuona Mungu; wakati mwingine wimbo kwenye redio unaweza kutimiza kitu hichohicho.
Kuhusu Mpango huu
Ni rahisi kuhisi kwamba umeelemewa, huna vifaa vifaavyo, na kwamba umepotea inapokuja kwenye Neno la Mungu. Lengo langu ni kurahisisha mchakato huu wa kujifunza Biblia kwa kukufundisha kanuni tatu za muhimu katika kujifunza Biblia. Jiunge leo na mpango huu na utagundua namna ya kusoma Biblia si kwa taarifa pekee, bali pia kubadilisha maisha yako!
More