Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jinsi ya Kujifunza Biblia (Misingi)Mfano

How To Study The Bible (Foundations)

SIKU 2 YA 5

Usomaji wa Biblia ni Tabial


Tunakuwa kile tunachokifanya mara nyingi. – Sean Covey


Ikiwa tunajua au la, maisha yetu yanasimama kwenye tabia zetu. Tunachokula, tunavyokabili msongo, ikiwa tunazima kengele ikiita ama la -yote haya yanaongozwa na tabia tulizoruhusu katika maisha yetu.

Mwandishi Charles Duhigg anaandika kwamba karibia 45% ya yote tunayoyafanya kwa siku, kila siku, ni tabia. Kama una tabia njema, basi hiyo inatia moyo. Lakini kama tabia zako haziko vile unavyotaka ziwe, basi hiyo maana yake nusu ya maamuzi ambayo ulikuwa na nafasi ya kuyafanya yalikuwa tayari yamefanywa kwa ajili yako ( na yamefanywa vibaya). 

Ninakwambia hayo kwa sababu ninataka ufahamu jinsi ilivyo muhimu mara kwa mara kusoma neno la Mungu.

Kwa nini watu wakuu wa imani tunaowaona katika maandiko walikuwa hodari? Kwa sababu kuwa na muda na Mungu na muda katika neno lake havikuwa vitu vya mjadala katika siku zao. 

Mbali na makosa yote aliyofanya Mfalme Daudi, alirudi kwa Mungu katika neno la Mungu, na kusahihisha maisha yake kulingana na neno linavyosema, na kuijenga historia ya Israeli kwa sababu ya neno.

Paulo aliishi kama Farisayo kweli kweli aliyeishi na kupumua maandiko. Na Yesu alipoyageuza maisha yake, alilikabili neno la Mungu na ujasiri mpya na alitimiza kusudi la maisha yake kwa sababu ya neno.

Kama kuna mtu angepata vema katika tabia ya Biblia kila siku, alikuwa ni Yesu. Kwani mara kwa mara tulimuona Yesu akitoroka ili kusoma neno na kuomba sehemu ya utulivu. Alielewa zaidi ya yeyote kati yetu, jinsi ubinadamu wetu unavyohitaji kuchochewa na kukutana na Mungu. 


Dondoo: Unasumbuka kusoma Biblia yako mara kwa mara? Fungua Biblia na uiache wazi ama karibu na mlango wa kuingia chumbani kwako au jikoni. Kwa njia hiyo, unapotoka kwenda kwenye shughuli zako za siku utasoma angalau mstari mmoja unapopita hapo. Lengo la kutengeneza tabia nzuri ni kuifanya kuwa rahisi (mstari 1) na kuona (tayari imefunguliwa kwenye njia yako).

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

How To Study The Bible (Foundations)

Ni rahisi kuhisi kwamba umeelemewa, huna vifaa vifaavyo, na kwamba umepotea inapokuja kwenye Neno la Mungu. Lengo langu ni kurahisisha mchakato huu wa kujifunza Biblia kwa kukufundisha kanuni tatu za muhimu katika kujifunza Biblia. Jiunge leo na mpango huu na utagundua namna ya kusoma Biblia si kwa taarifa pekee, bali pia kubadilisha maisha yako!

More

Tungependa kushukuru Faithspring kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.ramosauthor.com/books/