Jinsi ya Kujifunza Biblia (Misingi)Mfano
Kwa nini Kusoma Biblia ni Muhimu?
Haiwezekani kumjua Mungu pasipo kuifahamu Biblia.
Nakumbuka niliposikia kwa mara ya kwanza mstari huu. Nilikuwa mkristo mchanga nikiwa na shauku ya kuchagua kitu sahihi cha kuuongoza moyo wangu kwenye shauku sahihi. Nilijua Mungu anaweza kubadilisha maisha yangu na nilitaka kumjua kwa karibu.
Alikuwa anafananje? Alikuwa anataka nini kutoka kwangu? Kwa nini nilikuwa hapa?
Kwa karne iliyofuata, nilifanya kuwa ni wajibu wangu kujifunza Biblia kwa kadri ninavyoweza ili nimjue Mungu kwa undani zaidi. Uamuzi huo umenipeleka katika njia ambayo sikuweza kuifikiria.
Ibada hii fupi ni utangulizi wa ufahamu bora zaidi wa kutumia nilioupata kwa karne iliyopita. Utagundua mbinu, nyenzo, na mipango ya kukusaidia kupata kilicho bora katika muda wa usomaji wako, na pia kutiwa moyo kwamba kuijua Biblia yako ni thamani kwa kila juhudi inayohitajika kwa sababu mtoa zawadi ni Mungu mwenyewe.
Pata changamoto na jifunze namna ya kubadili ufahamu wako wa Biblia kutoka kwenye kazi na kuwa tabia muhimu. Mungu anakungoja umfahamu zaidi. Ameshatoa Mwaliko. Kinachofuata ni juu yako.
Kuhusu Mpango huu
Ni rahisi kuhisi kwamba umeelemewa, huna vifaa vifaavyo, na kwamba umepotea inapokuja kwenye Neno la Mungu. Lengo langu ni kurahisisha mchakato huu wa kujifunza Biblia kwa kukufundisha kanuni tatu za muhimu katika kujifunza Biblia. Jiunge leo na mpango huu na utagundua namna ya kusoma Biblia si kwa taarifa pekee, bali pia kubadilisha maisha yako!
More