Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku - HekimaMfano

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

SIKU 5 YA 5

Uoga wenye Hekima

Kuna uoga mwema. Kumuogopa Mungu ni moja yao. Ni jambo la msingi. Inalisha uoga wote mwema. Mwenye hekima ni mume ama mke ambaye kwanza anamuogopa Mungu. Kumuogopa Mungu ni kigezo kikuu mwanzoni wa matembezi yako ya imani. Ni wakati wa fungate katika ndoa yako na Kristo. Hujui vyema zaidi ya kutenda kile kinacho tarajiwa. Lakini kumuogopa Mungu kunapo puuzwa, unaingia bila kutaka katika hali ya kutotii. (Zaburi 36:1) Kama kuamini kwokwote kule ama utii. Kumuogopa Mungu kunakuwezesha kuwa mkweli Kwake na kwako mwenyewe. Ni mwanzo wa uwajibikaji. Neema ya Mungu - bila kumuogopa - ni mauzauza. Hakuwezi kuwa neema bila uoga, kama vile tu hakuna uoga bila neema. Mpumbavu ni yule asiye muogopa Mungu. Matunda ya kutomuogopa Mungu ni maamuzi ya kipumbavu na kuishi maisha bila kutii.

Ukiongezea, kufanikiwa ni adui ya kumuogopa Bwana. Unapozidi kufanikiwa, ndio una mwelekeo zaidi wa kutomuogopa Mungu. Hata hivyo, mbadala wake pia ni kweli. Unapofurahia mafanikio zaidi, ndipo unapopaswa kumuogopa Mungu zaidi na kuogopa mazao ya dhambi. Mafanikio, kwa mara nyingi, inakupatia utawala. Ni hapa utakua mwenye hekima kwa kuongeza uajibikaji. Kuwa mkweli kabisa kibinafsi. Huwezi kuwa na uhuru wa utawala bila uajibikaji. Daudi hakuweza, na alikuwa mtumishi aliyeutafuta moyo wa Mungu (Matendo 13:22). Utawala bila uajibikaji uletea msururu wa maamuzi mabaya, na ukiachwa bila mtazamo wa karibu, uelekeza tabia mbaya. Hakuna aliye juu ya sheria, na hakuna aliye juu wa uwajibikaji.

Kiongozi mwenye hekima, uweka uajibikaji katika imani yake, mapato, familia, kazini, na katika burudani. Wanaodhani hawaitaji uajibikaji ndio wanao hitaji zaidi. Labda unaanza kwa kumuajiri karani wa kibinafsi mwenye jinsia sawa na wewe kazini na katika safari za kibiashara. Hii ni nafasi ya kumshauri kama kiongozi anayekuwa, na ni nafasi yake kukuwezesha uwajibike. Sote tunafanya vyema wengine wanapotuangalia. Kumuogopa Mungu kunakusaidia kutofanya dhambi. ( Kutoka 20:20). Ukaribishe uajibikaji kutoka kwa mpenzi wako, baraza, bosi, na kikundi cha uajibikaji. Kuwa na uwazi na matumizi yako ya fedha kibinafsi na katika utenda kazi wako. Mweleze mpenzi wako unapojipata una utegemezi wa kihisia kwa mtu mwengine. Kuwa na uangalifu kwa wakati unao tumia ukiwa peke yako. Kutokua na jambo la kufanya uelekeza kutenda mabaya. Una hekima kuwekelea wakati wako wa upweke kwa Mungu, mpenzi wako, na rafiki wa karibu. Kumuogopa Mungu ni rafiki yako. Kuyaogopa matokeo ya dhambi ni kuwa mwerevu. Kuogopa kutokuwa na uajibikaji ni hekima. Kumuogopa Mungu ni kupata uhuru. Kwa hivyo, muogope Mungu, chukia dhambi, na muamini Mungu.

Kwa maelezo zaidi yaKuutafuta kila siku moyo wa Mungu, enda katika:

https://www.amazon.com/Seeking-Daily-Heart-Boyd-Bailey-ebook/dp/B0054RFUQS/ref=sr_1_2?ie=UTF8&qid=1538167375&sr=8-2&keywords=Seeking+Daily+the+Heart

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, "Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako."Biblia inasema, "Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote." Zaburi 119:2 (BHN)

More

Tungependa kushukuru Boyd Bailey akishirikiana na Wisdom Hunters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kwa: https://www.wisdomhunters.com/