Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku - HekimaMfano

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

SIKU 1 YA 5

Wanaotafuta Hekima

Hekima ni kitu cha dhamana. Watu huvutiwa na hekima. Inapendeza na yenye kuvutia. Hekima inawakilisha neno kutoka kwa Mungu, kwa hivyo umuhimu wake ni mkuu. Hekima ni sababu moja tunaenda kanisani, tunasikiza mahubiri mema, na kuwahusisha washauri wakongwe. Hekima lazima itafutwe na kuuluziwa. Haiji tu kwa ukawaida, ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hekima ni ya dhamana na umuhimu mkuu. Ni zawadi inayo kulinda kutokana na maamuzi yatakayo kusumbua maishani mwako na kukupa ujasiri wa kuendelea ama kuacha. Hekima ni silaha Mungu huitumia kwa niaba ya mashujaa wake. Hekima inatoa sintofahamu na kukuletea uwazi. Ina tafsiri maamuzi katika mfululizo wa ushindi mdogo mdogo. Ina kutahadharisha dhidi ya hatari.

Wenye hekima, hata hivyo, hawana kinga dhidi ya dhambi. Mwenye hekima bado anahitaji uajibikaji - zaidi. Kwa kweli, wenye hekima wana urahisi wa kujigamba (Jeremia 9:23). Moyo wenye hekima na kujigamba hudhania unaweza inuka dhidi ya sheria. Mwanzo wake ni mdogo usio onekana kama hatari lakini uzidi na kuwa msingi mbaya zaidi. Kama kujigamba kwa wenye hekima hakuta angaliwa kutageuka kuwa kujiona bora kuliko wengine. Inasikitisha kuwaona viongozi ambao wakati mmoja walimuogopa Mungu lakini sasa wemejawa kiburi. Hekima ni zawadi ya Mungu kufanikisha matakwa yake ya mbinguni. Hekima ikitumika vibaya, inatusaidi sisi tu.

Kwa hivyo watafute wenye hekima ya kweli, walio kiweka kigezo chao kwa Mungu peke yake. Hekima yenge kiburi husababisha maafa ya kiroho, lakini hekima safi uleta uzima katika maisha ya kiroho. Ni hekima, pamoja na upole na kumtii Mungi - inayo tutayarisha kumaliza vyema. Hekima ya kweli ni bora katika hali zote. Itafute hekima hii katika Biblia, vitabu, watu, hali, filamu, maishani na katitaka maumbile. Unapo ipata, usiichukulie kwa mzaa. Badala yake mshukuru Mungu kwa matokeo yenye hekima. Itumie kumtukuza Mungu na kukamiliza matakwa yake. Ruhusu hekima ikunyenyekeze na wala sio kujiona kuwa mkuu kuliko wote. Sote tunaitafuta hekima ya Mungu. Tutaitafuta hadi tufike mbinguni.

Hekima ina vitendo, uhai na inahitaji kujazwa kila mara kutoka kwa Mungu. Tumia maombi kama daraja kuifikia hekima ya Mungu. Muulize Mungu kila mara mawaz yake na nia yake katika kila jambo. Ruhusu hekima ikulete karibu na Mungu wa mbinguni unapozidi kumuabudu na kumtegemea kwa kila jambo. Imarisha matakwa na hekima yako mbele zake. Muweke Mungu wako kama kichungi chako unapozidi kufunya maamuzi yenye busara.

Wagawie wengine hekima yako bila ubaguzi, fanya vikao na wengine ili waufahamu moyo wako na kuelewa mafunzo makuu Mungu amewezesha katika maisha yako. Sote tuna busara tunayoweza kuwapa wengine. Chukua mda kuyaelewa masaibu ya wengine. "Mambo yao Makuu" yanayohitaji hekima yako. Kuwa tayari kusikiliza kwa umakini, bila haraka na ujaribu kuelewa, na kwa upole uwape uchaguzi baina ya suluhisho tofauti tofauti. Hekima ina upole. Inapeana majibu kwa wote katika roho ya ukarimu na neema, ikifahamu sote tunatafuta hekima.

Tafuta na Upeane Hekima - hekima kutokana na kujitolea kwa upole mblele za Mungu.

Kwa matoleo zaidi kutokaKuutafuta Moyo wa Mungu kila siku, tembelea tovuti:https://www.wisdomhunters.com/

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, "Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako."Biblia inasema, "Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote." Zaburi 119:2 (BHN)

More

Tungependa kushukuru Boyd Bailey akishirikiana na Wisdom Hunters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kwa: https://www.wisdomhunters.com/