Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku - HekimaMfano
Utajiri wa Hekima
Hekima ni kama hela. Thamani yake inaongezeka maradufu wakati unapozidi kuongezeka. Ukiongeza hekima kila mara katika maisha yako, unakua tajiri katika njia za Mungu. Ndio mana ina umuhimu zaidi upate hekima zaidi ya vitu vyote katika maisha yako. Hekima ni kipaji cha kuweza kubainisha mema na mabaya na kuelewa kilicho cha kweli na kitakacho dumu. Ni rafiki yako atakaye kusaidi kumshinda adui. Shetani hana makali yeyote mbele ya hekima ya Mungu. Usijaribu kumshinda shetani kupitia kuelewa kwako kwenye kipimo kichache. Badala yake, mshinde kwa uzito ukitumia hekima. Maisha yaliyojengwa kwa msingi wa hekima yanaweza dhibiti upepo wa mabadiliko na wawimbi ya dhiki. (Mithali 28:26). Hekima inakuweka katika maono ya Mungu. Inayalinda maisha yako dhidi ya kuzama, na kukupatia mwelekeo unapopotea, na kukumulikia njia katika giza na mambo usiyo yaelewa kwa ukamilifu.
Hekima ni kama dhahabu, na dhahabu sio rahisi kupata. Kuna gharama ya kulipa. Kuna gharama ya kulipa katika harakati ya kuipata na kuiifadhi (Mithali 16:16).
Kuwepo kwa nywele za kijivu sio ishara ya hekima, lakini uzoefu wa kupitia hali tofauti tofauti unakuweka katika nafasi ya kupata hekima. Inawezeka uwe mzee mpumbavu ama uwe na hekima kupita miaka yako. Ukiwa kijana ama mzee, mwerevu ama mwenye kuelewa kwa kimsingi, kwa yote haya, unaweza kupata hekima.
Hekima uanza na kuisha na kumuogopa Mungu. Kumuogopa Mungu kuna maana unayawekea uzito mafunzo yake moyoni na akilini mwako. ( Mithali 15:33). Hekima ni uhusiano wa karibu na wa kila mara na Mungu. Hekima inamaanisha unatafakari njia Zake na kuishi katika ukweli. Unamuuliza kwa maombi na heshima, kwa nini, ni nini, na vile mambo yana usiano na njia zake za kufanya mambo. Kama wafwasi wa Mungu, tuna akili ya Kristo. Kwa kutafakari neno lake na kuelewa ukweli wake hekima itaanza kuchukua hatamu katima maisha yetu ya kila siku. Kwa neema ya Mungu, hekima itatuwezeka kupambana na machaguzi mengi na kubaini njia mwafaka zaidi ya kufanya mambo.
Hekima inaweza kuchukua jambo gumu na kukupa jibu la urahisi. Hekima inaweza baini jambo la muhimu zaidi katika mkusanyiko wa ushawishi na matakwa mengi. Hekima ni mwakilishi asiye kejeli kwa ustaarabu na ukweli. Hekima ina urahisi wa matumizi.
Hekima hutoka kwa Mungu na inaishi ndani yake. Ana chapa na leseni yake. Yeyote anayetaka kuchukua pongezi kwa matumizi bora ya hekima huenda akaipoteza nafasi ya kuitumia. Unyenyekevu ukifuatana na hekima huelekea maamuzi bora. Chukua wakati kusikiza na kujifunza kutoka kwa watu wenye hekima. Hii inaweza kukunusuru kutoka kuvunjwa moyo kutotakana na mahusiano, na kupoteza hela kutokana na maamuzi mabaya. Kuwa na hekima; wasikilize wote Mungu na washauri wenye hekima
Unapata hekima ili upatiane hekima, na kugawa utajiri wa hekima na wale watakao itumikia vyema.
Kuhusu Mpango huu
Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, "Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako."Biblia inasema, "Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote." Zaburi 119:2 (BHN)
More