Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku - HekimaMfano

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

SIKU 2 YA 5

Mwito wa Hekima

"Hii inahitaji hekima" (Ufunuo 13:18a). Hekima huitajika mara zaidi ya vile tunavyodhania. Hekima hutenganisha hisia na kufikia ukweli kamili wa jambo fulani. "Ni jambo lipi la busara la kufanya?" ni swali mwafaka katika kufanya maamuzi. " Ni jambo lipi jema zaidi la kufanya katika biashara yangu? ni swali lenye hekima kuuliza katika biashara na utumishi wako. Mara nyingi Mungu uongea nasi kupitia kuwapo ama kutokuwa hela katika maisha yetu. Kwa hivyo kama hela imebana, basi tunahitaji kuwa waangalifu katika matumizi yetu. Hekima inatuambia tupunguze matumizi na tusiongeze gharama zengine. Wakati huu, sio ukosefu wa imani. Ni kuhusu kuwa na busara na kidogo ulichonacho, ili uweze kuaminika na vingi. Utumizi wa mapato kwa hekima huwavutia wanaotoa kwa wingi.

Wenye hekima hawana haraka na hawa papatiki. Hekima huchukua mda kutafsiri jambo kabla ya kuamua cha kufanya. Je, unatafuta busara kila mara? Kufahamu na uzoefu wa maisha ukichanganya na akili timamu na kufahamu ni mchanganyiko mzuri kwa hekima. Hekima nikujaribu kuelewa mawazo ya Mungu katika mambo. Hii ndio sababu kuu kwa nini hekima inayopatikana katika neno la Mungu ni ya maana zaidi kwa maisha yetu leo.

Biblia ni hazina ya kauli na hekima inayo gonja kupatikana na wale wanaotafuta hekima katika maisha yao. Kwa hivyo usiombe, kusoma na kutafakari Biblia tu, ila itafute hekima (Mathayo 12:42). Watafute watu wakongwe, wanao onyesha tabia zenye hekima. Wenye busara hawa watakusaidia kuwa na hakikisho katika busara unayozidi kuipataka katita Neno. Soma vitabu na usikilize jumbe tofauti kutoka kwa wanawake na wanaume wenye busura. Ukitumia mda mwingi na hekima, utakua na hekima. Chukua nafasi yoyote ile unayo kupata hekima. Kuwa na hekima katika mahusiano yako. Kuwa na hekima katika fedha na wakati wako. Kabla hujagundua, wengine watapendezwa na kuvitiwa na hekima yak.

Basi, ukuu wa hekima ni kumuoogopa Mungu. "Kumuogopa Mungu ndio mwanzo wa hekima lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu" (Methali 1:7). Kumuogopa Mungu hukuweka katika nafasi ya kupokea hekima. Usipo muogopa Mungu inamana huna hekima. Ndio mana ulimwengu umejaa wapumbavu. Tumeupoteza uoga wetu kwa Mungu, na hekima imetutoweka. Kumuogopa Mungu ni kuifadhi hekima. Mungu anawapa hekima wale wanao muogopa.

Mpende Mungu, lakini Muogope. Muabudu Mungu, lakini Muogope. Jifunze kutoka Kwake, lakini Muogope. Mtumikie Mungu, lakini Muogope.

Kumuogopa Mungu kuna kupa kibali cha kupata hekima. Usipate uzoefu na Mungu hadi upoteze Kumuogopa. Hio ni kukosa hekima na unakuogoza katika ujinga. Hekima inagojea wito wako. Vuna na ufurahie, kama tunda zuri katika msimu wake. Onja na uone hekima ni tunda zuri. Hakuna hata mmoja aliye lalamika kupata hekima kupita kiasi. Utafute hekima, muulize Mungu akupe hekima. Hili ndilo jambo la busara kufanya.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, "Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako."Biblia inasema, "Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote." Zaburi 119:2 (BHN)

More

Tungependa kushukuru Boyd Bailey akishirikiana na Wisdom Hunters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kwa: https://www.wisdomhunters.com/