Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuutafuta Moyo wa Mungu kila Siku - HekimaMfano

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

SIKU 3 YA 5

Hekima kutoka kwa Unyenyekevu

Hekima imejaa unyenyekevu. Ni kama mapacha. Unyenyekevu umejaa maudhui mengi mema. Na hekima ndio moja ya maudhui yake makuu. Ukitaka hekima lazima uwe mnyenyekevu moyoni. Unyenyekevu ufikisha hekima kama dereva amfikishavyo abiria sehemu aendako. Wanasafari pamoja. Kwa njia moja hekima upea kipao mbele unyenyekevu. Wanyenyevu wanaielewa haja yao ya hekima kutoka kwa Mungu. Siku zimepita kwa nyakati ambazo ungejifanya unayafahamu yote. Unyenyekevu unakiri uhitaji mawazo ya Kristo kuchanganyika na ufahamu wetu. Unyenyekevu wa kweli unakiri yale usiyo fahamu.

Mambo mengi maishani yamepita kwa umbali ufahamu wa mwanadamu. Lazima kuwe na zaidi ya ufahamu wa binadamu. Hatuna lengo na ufahamu wa kutosha kuweza kufanya uamuzi unaofaa kwa kuelewa kwetu tu. Tunahitaji hekima ya Mungu kuosha mawazo yetu na kutuacha na upako wake wa utakatifu. Unyenyekevu unatuweka katika nafasi ya kupokea hekima kutoka kwa Mungu na wengine. Ni katika harakati ya kukomaa. Hata Yesu alizidi katika hekima (Luka 2:52).

Kiburi kinakutoa katika nafasi ya kupokea hekima. Ni kama mchezaji aliye nje ya uwanja mechi inapoanza. Hataweza kufunga bao mchezo unapoanza. Bila unyenyekevu haopo katika nafasi ya kupokea hekima. Unaweza hata tamani kupata hekima, lakina bila unyenyekevu, utakosa katika nafasi ya kupata maelekezo kutoka mbinguni. Mungu kwa nadra sana anaelekeza hekima yake kwa mtu mwenye kiburi kwa sababu Anajua mtu mwenye kiburi haaminiki. Kwa nini umpe hekima mtu ambaye ataitumia hekima hiyo kujiboresha peke yake? Mungu anafahamu mtu mnyenyekevu moyoni ataitumia hekima kwa njia bora. Kwa kweli, unyenyekevu unaiweka njaa ya hekima moyoni. Inatupa matarajio makuu na ya kipekeee ya kutaka hekima maisha mwetu.

Mara tu unapo yageuza majarajio yako kupokea hekima, hautarudia mankuli duni ya hekima inayotoka ulimwenguni. ( 1 Wakorintho 1:20-30). Hekima ya ulimwengu ipo ndani ya kiburi. Ni kujipiga kifua kati ya nani aliye mjanja zaidi anayeweza kuwapita kimawazo wapinzani wote. Kila kitu ni mashindano kwa walio na kiburi. Kwa ujinga mwingi anaitafuta kwa nguvu nafasi ya kuwa mbele ya wote. Wanyenyekevu, nao, humgojea Mungu. Kuna undani na ukakamavu unaozalisha hekima itokayo ndani ya kujinyenyekeza mbele za Mungu. Aibu ndio ndugu wa karibu wa kiburi. Kiburi kinaweza kukupa unachotaka, lakini kukuletea aibu kwa siku zijazo.

Heri kunyenyekea na kufuata njia ya hekima. Hekima inakuruhusu kupumzika vyema; hekima inakupa neema; hekima inakupatia matokeo bila majuto. Kwa hivyo, kwa unyenyekevu ukaribishe hekima ya Mungu katika maisha yako.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Seeking Daily The Heart Of God - Wisdom

Kuutafuta Kila Siku Moyo wa Mungu ni Mpango wa Siku 5 wenye madhumuni ya kututia moyo, kukupa changamoto na kukusaidia kuishi maisha ya kila siku. Kama mwandishi Boyd Bailey alivyosema, "Mtafute wakati wote bila kujali hisia, hata ukiwa na kazi nyinyi, Mtafute Mungu naye ataubariki uaminifu wako."Biblia inasema, "Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote." Zaburi 119:2 (BHN)

More

Tungependa kushukuru Boyd Bailey akishirikiana na Wisdom Hunters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kwa: https://www.wisdomhunters.com/